Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 2nd, 2021

 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 02/02/2021.

Mikoa ya Kigoma, Katavi,Kagera na Geita: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, Mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.............
Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu na Tabora: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Songwe na Iringa: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo
machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga (Visiwa vya Unguja na Pemba),Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
............
VIWANGO VYA JOTO,VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 30°C 13°C
D'SALAAM 33°C 25°C
DODOMA 30°C 19°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 24°C 14°C
IRINGA 27°C 15°C
NJOMBE 20°C 12°C
MWANZA 30°C 20°C
TABORA 30°C 19°C
TANGA 32°C 23°C
ZANZIBAR 32°C 24°C
...........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Alhamisi tarehe 04/02/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 02/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments

Powered by Blogger.