Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 21st, 2021

 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 21/02/2021.

Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa,: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
..........
Mikoa ya Kilimajaro, Arusha na Manyara: Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Morogoro, Lindi, Mtwara, Dar es salaam, Tanga, Pwani ( ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba: Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Dodoma na Singida: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es
Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango chachini
cha joto cha joto
ARUSHA 27°C 17°C
D'SALAAM 30°C 25°C
DODOMA 29°C 19°C
KIGOMA 26°C 20°C
MBEYA 29°C 17°C
IRINGA 27°C 17°C
NJOMBE 21°C 12°C
MWANZA 24°C 22°C
TABORA 28°C 19°C
TANGA 34°C 24°C
ZANZIBAR 31°C 25°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 23/02/2021: Mabadiliko madogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 21/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments

Powered by Blogger.