Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 22nd, 2021

 

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:

TAREHE: 22/02/2021.

Mkoa wa Ruvuma, Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Manyara, Kilimanjaro, Arusha pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

..........

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kigoma, Tabora,  Katavi, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam,Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara,   Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na 

Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

...........


ANGALIZO

VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO NA

MANYARA.


VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:


MJI                Kiwango cha juu       Kiwango cha chini

                      cha joto                    cha joto

ARUSHA        25°C                         17°C 

D'SALAAM     31°C                         25°C 

DODOMA      29°C                         19°C 

KIGOMA        29°C                          20°C 

MBEYA           29°C                         16°C 

IRINGA           27°C                         17°C 

NJOMBE         21°C                         12°C 

MWANZA       26°C                         22°C 

TABORA          27°C                        18°C 

TANGA            32°C                        25°C 

ZANZIBAR       32°C                        25°C

.........


Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani yote.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.

Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 24/02/2021: 

Mabadiliko Kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 22/02/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa siku Tano

Jumatatu: Tarehe 22-02-2021

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI


ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: MDOGO

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: KIKUBWA.


Athari zinazoweza kujitokeza: Makazi kuzungukwa na maji pamoja na kucheleweshwa kwa shughuli za usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

...........


Jumanne 23-02-2021

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI


Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kucheleweshwa kwa shughuli za usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

...........


Jumatano 24-02-2021

HAKUNA TAHADHARI


Alhamisi 25-02-2021

HAKUNA TAHADHARI


Ijumaa 26-02-2021

HAKUNA TAHADHARI

Post a Comment

0 Comments