Mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, Kagera, Geita, Mwanza, Tabora, Kigoma, Katavi, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Rukwa na Ruvuma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, Mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.............
Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.............
Mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mkoa wa Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
.............
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 29°C 16°C
D'SALAAM 32°C 24°C
DODOMA 31°C 20°C
KIGOMA 28°C 20°C
MBEYA 28°C 18°C
IRINGA 27°C 16°C
NJOMBE 20°C 12°C
MWANZA 29°C 19°C
TABORA 31°C 19°C
TANGA 33°C 24°C
ZANZIBAR 33°C 25°C
............
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya jumapili tarehe 07/02/2021: Mabadiliko Kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 05/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.