Vyama vyaendelea kujengewa uwezo namna ya kujaza fomu za marejesho gharama za uchaguzi

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa(ARPP), Sisty Nyahoza akisisitiza jambo mbele ya washiriki wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi Februari 25, 2021 katika ukumbi wa Samwel Sitta zilizopo Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi kutoka Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Chama cha Kijamii (CCK).Kulia ni Mwenyekiti wa mafunzo hayo Bi. Hollo Kazi.
Kaimu Msajili Msaidizi anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo Kazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 jana jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yameudhuriwa na viongozi kutoka Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Chama cha Kijamii (CCK).Kushoto ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (ARPP), Bw. Sisty Nyahoza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Maajaliwa Kyara akichangia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Mafunzo hayo yameudhuriwa na viongozi kutoka Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Chama cha Kijamii (CCK).
Mhasibu waa Chama cha Kijamii (CCK) akichangia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Mafunzo hayo yameudhuriwa na viongozi kutoka Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Chama cha Kijamii (CCK).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 leo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yameudhuriwa na viongozi kutoka Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Chama cha Kijamii (CCK). (Picha zote na ORPP).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news