Wanawake wahamasishwa kujijengea ujasiri kuingia vyombo vya maamuzi

Wanawake wametakiwa kutambua kuwa,licha ya wengi wao visiwani Zanzibar kushindwa kushika nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu uliopita 2020, bado hawapaswi kukata tamaa badala yake wanaombwa kuendelea kujijenga katika kushika nafasi hizo na nyingine katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanaume wa mabadiliko waliopatiwa mafunzo kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa-Zanzibar) jijini Zanzibar.
 
Mafunzo yaliyotolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa lilojihusisha na haki za wanawake (UN Women), yenye lengo la kuwainua wanawake wa Zanzibar waweze kushiriki katika vyombo vya kutoa maamuzi mkutano uliofanyika ukumbi wa watu wenye ulamvau kikwajuni mjini Unguja.

Akitoa taarifa ya awali kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassan Jani amesema baadhi ya watu bado kwenye jamii hawajatoa kipaumbele dhidi ya wanawake na uongozi na kwamba wanahitaji kubadilishwa ili waweze kutoa fursa zaidi na kuwaunga mkono wanawake.

Amesema, licha ya kazi kubwa ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea katika uchaguzi uliopita lakini wanawake wengi wameshindwa kufikia malengo ya kuwa viongozi kutokana na sababu mbali mbali.

Akitaja baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kutokuwepo kwa mshikamano kwenye jamii ambapo alieleza kuwa mshikamano ndio njia kuu ambayo ingeweza kuwainua wanawake wote waliogombea.

Akifafanua zaidi amesema suala la mshikamano na mani katika maeneo mbali mbali yatawezesha wanawake wengi kukubalika na kujengewa uwezo sambamba na kuendelea kuelimisha zaidi jamii kuona umuhimu wa kuwaunga mkono wanawake.

Katika hatua nyingine alisema wakati maeneo mengi yakiendelea kusubiri uteuzi wa masheha wapya wakuu wa mikoa wana wajibu wa kulitazama suala hilo pia na umuhimu wa ushiriki kwa wanawake katika uteuzi huo wa masheha wapya.

Pamoja na hayo amesema licha ya uwepo wa harakati za kuwawezesha wanawake katika nafasi za uongozi lakini bado baadhi ya wanajamii wana uelewa mdogo na kuhisi wanawake hawapaswi kuwa viongozi.

Wakati hayo yakijiri mshiriki mwingine kwenye majadiliano hayo Almas Mohamed Ally amesema, kuna haja ya kutengeneza mazingira ya ushawishi katika ngazi za juu za chama badala kujengewa uelewa wananchi kwa kuwa vyama vya siasa navyo vina maamuzi yao kuwapitisha wagombea.

Sambamba na hayo alivitaka vyama vya siasa kuhakikisha nafasi za uteuzi kuwatazama zaidi wanawake ambao waliwahi kujitokeza kugombea licha ya kutofanikiwa kwao.

‘’Iwapo mazingira haya yatafanyika kupewa nafasi za uteuzi kwa wanawake waliogombea bila shaka idadi kubwa zaidi itaendelea kujitokeza wakiamini kuwa kugombea kwao hwenda ikawa fursa ya wao kupanda na kuwa viongozi,"ameongeza.

Kwa upande wake Ukhty Amina Salum Khalfan kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar amesema, Zanzibar kuna baadhi ya watu kwenye jamii wakiwemo viongozi wa dini wamendelea kuwa na mtazamamo wa kuwakandamiza zaidi wanawake na kuhisi hawapaswi kuwa viongozi.

Amesema hakuna sehemu yoyote hile katika vitabu vya dini iliokataza wanawake kutokuwa viongozi badala yake imewekwa wazi kuwa wanawake wanapaswa kushirikishwa katika uongozi na kutoa maamuzi.
 
Ukhty ametoa wito kwa jamii kuacha mtazamo wenye lengo la kuwakandamiza wanawake wakidhani ni watu wanaopaswa kubaki ndani pekee wakati wanawake ndio wenye jukumu kubwa la ulinzi wa familia kazi ambayo hata wanaume wengi wanashidwa kuifanya katika jamii mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news