Waziri Gwajima: Naagiza asimamishwe kazi mara moja

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima ameagiza kusimamishwa kazi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chunya, Dkt. Felista Kisandu kwa kukiuka mwongozo wa utoaji wa taarifa za milipuko kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya Afya ya Umma ya mwaka 2009.
Akitoa tamko Februari 7, 2021 Dkt. Gwajima amesema, Dkt. Kisandu anapisha uchunguzi kufuatia sakata la kusambaa kwa taarifa ya mlipuko wa ugonjwa usiofahamika kata ya Ifumbo wilayani Chunya.

“Kutokana na kadhia hii ambayo imeleta taharuki isiyo ya lazima naiagiza mamlaka ya ajira ya Dk Felista Kisandu ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chunya ichukue hatua za kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi chini ya Baraza la Madaktari na taarifa nipate ndani ya siku 10,” amesema Dkt Gwajima.

Amesema katika Kata ya Ifumbo, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya hakuna mlipuko wa ugonjwa wowote uliothibitishwa wala hakuna janga lolote la kiafya kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari.

Amesema, timu ya wataalamu imefanya mahojiano na wananchi na kubaini hakuna vifo 15 kwa mara moja vya wagonjwa wanaodaiwa kuwa na dalili za kutapika damu kama ilivyoripotiwa na diwani wa Kata ya Ifumbo na takwimu hizo hazijawahi kuripotiwa popote ndani na nje ya mji huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news