Waziri Mkuu azindua Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2020

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mwaka wa Fedha Unaoishia 30 Juni, 2020 baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, jana, Februari 9, 2021. Majaliwa pia alifungua Maonesho ya Nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Iddi Kimanta nakala ya Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mwaka wa Fedha Unaoishia 30 Juni, 2020 baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, jana..
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioshiriki katika Maonesho ya Nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi baada ya kufungua maonesho hayo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, jana, Februari 9, 2021. Majaliwa pia alizindua Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mwaka wa Fedha Unaoishia 30 Juni, 2020. Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dk. Festus Limbu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mgwira na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha Zelothe Steven.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa Mkoa wa Arusha kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, jana, Februari 9, 2021. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news