WAZIRI MKUU: TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU NA TUCHUKUE TAHADHARI

Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa amesema Watanzania wanaweza kuushinda ugonjwa wa corona kwa kumuomba Mungu na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya kuhusu njia za kujikinga na ugonjwa huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika maziko yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu).

“Katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na wimbi la ugonjwa wa mlipuko, la muhimu kwetu ni kuendelea kumuomba Mungu kama Mheshimiwa Rais alivyotuasa tufunge kwa maombi ya siku tatu; Ijumaa kwa Waislamu kama walivyofanya, Jumamosi kwa Wasabato tumeona mwitikio wao na kwa Wakristo kesho Jumapili kama tulivyoona maandalizi yakifanyika,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, leo Februari 20, 2021, Waziri Mkuu amesema: “Pamoja na kumuomba Mungu, ni lazima tuendelee kufuata maelekezo ya kitaalam ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, tutumie vitakasa mikono na kuvaa barakoa.”

Kuhusu uvaaji wa barakoa, Waziri Mkuu amesema Serikali haijazuia mtu kujikinga lakini aliwataka wanaozitumia ni lazima wajiridhishe na ubora, usalama wake na wafahamu zimetoka wapi. 

“Ni lazima wanaozitumia wajue zimetoka wapi. Ni vema watu washone barakoa zao wenyewe au wanunue zilizotengenezwa na viwanda vya Tanzania kama alivyoshauri Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mwaka jana.”

Amesema: “Pamoja na maombi, Watanzania tunapaswa tuendelee kufuata maelekezo ya Serikali bila kuwa na hofu. Serikali kupitia maabara na vituo vya kutoa huduma, inaendelea kuhakikisha huduma zinapatikana.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Francisca Kijazi, Mjane wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi John Kijazi katika Ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Mawaziri wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustino, eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi hayo. Kutoka kushoto ni , Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Juma Aweso, Waziri wa Maji, Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesugulikia Muungano na Mazingira, Profesa Joyce Ndalicako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia na kulia ni Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Aksoni akiwekashada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika Mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021.
 
Akimzungumzia marehemu Balozi Kijazi, Waziri Mkuu aliwapa pole wafiwa na wanafamilia kutokana na msiba huo mkubwa na akamuelezea kwamba, alikuwa kiongozi mwenye mapenzi mema na Taifa lake lakini pia alikuwa na uwezo wa kutoa ushauri ambao ulikuwa na manufaa kwa Taifa. “Tunalo jukumu la kumuenzi kwa kuendeleza na kutenda mema yote aliyotuachia.”

Ibada ya kumuombea Marehemu Balozi Kijazi ilifanyika katika kanisa la Mt. Agustino, eneo la Manundu, mjini Korogwe, mkoani Tanga na iliongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphory Mkude.

Mapema, akizungumza katika mazishi hayo, Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo alisema wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa karibu naye kwa sababu Balozi Kijazi alikuwa ni Katibu wa Baraza la Usalama la Taifa.

“Alikuwa ni mahiri, mpole na mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ambazo zilieleweka na kukubalika katika vikao vyao,” alisema.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Martine Shigela alisema Balozi Kijazi alikuwa ni Baba, kiongozi na mwalimu na wakati wote alikuwa ni kielelezo cha uchapakazi na uadilifu kwa watu wa mkoa wa Tanga. “Na kwa sababu hiyo, mkoa umeamua kuwa stendi ya mabasi ya mji wa Korogwe itaitwa jina la Balozi John Kijazi kwa heshima yake na ili kutunza kumbukumbu yake,” aliongeza.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na Wabunge wa mkoa wa Tanga.

Mhandisi Balozi Kijazi alizaliwa mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto 10. Ameacha mke, watoto watatu pamoja na wajukuu wawili

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news