Waziri Ummy: Tutatoa mafunzo ya wabunge, wakurugenzi na viongozi Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Ummy Mwalimu ameahidi kutoa mafunzo ya pamoja kati ya Wabunge, Wakurugenzi na Viongozi wa Halmashauri kwa upande wa Zanzibar ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu usimamizi wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, anaripoti Lulu Mussa (Dodoma).

Amebainishwa hayo hii leo katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma, baina ya wabunge wa Zanzibar na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kujadili namna bora katika kufanikisha utekelezaji wa fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akifungua Kikao kazi cha Wabunge wa Zanzibar kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akitoa neno wakati wa kikao kazi cha Wabunge wa Zanzibar kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
Amesema kumekuwa na changamoto katika kuratibu fedha za kuchochea maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kwa upande wa Zanzibar na kuwahakikishia wabunge kuwa Ofisi yake itaangalia namna bora katika kufanya marekebisho ya Sheria ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

“Nimesikiliza changamoto zilizoainishwa naahidi kuwasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho ya mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo na kuratibu mafunzo ya pamoja ili wananchi wetu waweze kunufaika na fedha zinazotolewa kwa ufanisi na wakati” Ummy alisisitiza.

Pia, Waziri Ummy amewahakikishia wabunge hao ushirikiano katika kuratibu masuala ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano.
Sehemu ya wabunge kutoka wakifuatilia kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali wakati wa Kikao kazi cha Wabunge wa Zanzibar kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Mbunge wa Jimbo la Jang’ombe Ali Hassan Omar (King).
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Donald Chidowu akitoa mada wakati wa kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.

Kwa upande mwingine mmoja ya Wabunge kutoka Zanzibar Mhe. Ali Hassan Omary (King) kutoka Jimbo la Jang’ombe amesema Mabadiliko ya Sheria kuhusu Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo na kikao baina ya Watendaji wa Halmashauri na Wabunge wa Zanzibar vitatoa suluhu kwa changamoto zilizopo hivi sasa.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amesema kikao hicho kimekuwa cha manufaa na hazina kubwa sana katika kuratibu masuala ya Muungano.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Cesilia Nkwamu akitoa mada wakati wa kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI Sigbert Kaijage akitoa mada wakati wa kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muunganio na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo pamoja na wabunge wa Zanzibar na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma Januari 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muunganio na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.
  “Kwa kuwa Sheria hii ya kuchochea maendeleo ya Mfuko wa Jimbo imekuwa ya muda mrefu toka mwaka 2009, wataalamu watakaa ili kuangalia kama iko haja ya kutengeneza kanuni pia tutapeleka mapendekezo kwa wenzetu wa TAMISEMI ili iweze kufanyiwa marekebisho” Mhandisi Malongo alisisitiza. Sehemu ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakifuatilia kikao kazi kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma leo Januari 9, 2021.

Katika kikao hicho mada tatu zimewasilishwa ikiwa ni pamoja na Sheria ya Mfuko wa Jimbo, Usimamizi na Utekelezaji wa Fedha za Mfuko wa Jimbo na Changamoto za Mfuko wa Jimbo Zanzibar na Maoni ya kukabiliana nazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news