Wizi wa dawa za Hospitali wamtia hatiani Mhudumu wa Afya


"Siku hiyo ya tarehe 17,Desemba mwaka 2020 akiwa katika ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Kyela alionyesha hali ya wasiwasi iliyopelekea kumfanyia upekuzi kwenye begi lake alilokuwa nalo na kumkuta na dawa mbalimbali, mali ya Hospitali ya Wilaya ya Kyela. 

"Baada ya kumkuta na dawa hizo upekuzi zaidi ulifanyika nyumbani kwake na kwa kuhusisha uongozi wa Hospitali ya Wilaya ambapo walifanikiwa kukuta dawa na vifaa vya hospitali ya wilaya. Mhudumu huyo kwenye mahojiano na TAKUKURU alikiri kuiba dawa hizo,"Hayo yamebainishwa leo Februari 9, 2021 na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, Julieth Matechi.

No comments

Powered by Blogger.