Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA awashukia wanaoghushi hati za umiliki

Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare atoa onyo kali kwa Watayarishaji wa Filamu nchini wanaoghushi Hati ya Umiliki Halali wa Ubunifu “Clearance Certificate”,anaripoti Anitha Jonas (COSOTA) Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare akitoa onyo kwa Watayarishaji wa Kazi ya Filamu nchini kuacha kughushi Hati ya Umiliki halali wa ubunifu “Çlearance Certificate’’ wanapowasilisha kazi za filamu katika sehemu mbalimbali kwani hilo ni kosa la jinai leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Multichoice wa kutangaza fursa ya kutoa ufadhili kwa Waandaji wa Filamu nchini.

Mtendaji huyo ametoa onyo hilo leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Multichoice Tanzania uliolenga kutangaza fursa kwa Watayarishaji wa Filamu kuwasilisha andiko la Uandaaji wa Filamu ambapo Multichoice watatoa ufadhili wa fedha katika kuandaa kazi hiyo.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Bibi. Doreen alisisitiza kuwa hivi sasa ofisi yake tayari imeanza kutumia Kanuni ya Ufifilishaji, hivyo kwa wale watu wote watakao kamatwa wakifanya uharamia wa kazi za Sanaa wataadhibiwa kwa kanuni hii ambapo watahitajika kulipa faini isiyopungua milioni ishirini.

“Kumekuwa na baadhi ya watoa huduma za “Cable” kuwa na tabia ya chukua chaneli/vipindi zikiwemo filamu na tamthilia kutoka visimbuzi vingine au kutumia njia nyingine kurusha cable zao bila idhini ya wamiliki ya wamiliki wa maudhui hayo hili ni kosa sababu ni wizi na ukiukwaji wa Hakimiliki,”Bibi.Doreen.
Meneja Masoko na Uhusiano Multichoice Tanzania Bw.Ronald Shelukindo akitangaza fursa ya ufadhili kwa Waandaaji wa kazi za Filamu nchini katika mkutano na wadau wa filamu leo Jijini Dar es Salaam ambapo maandiko hayo yataanza kupokewa kuanziwa Machi 08 – 14, 2021.

Kwa upande wa Meneja Masoko na Mahusiano Multichoice Tanzania Bw.Ronald Shelukindo alisema utaratibu wa kupokea Maandiko ya Filamu utanza kuanzia tarehe Machi 08 hadi 14, 2021 na maombi hayo yatawasilishwa kwa njia ya tovuti, lengo la kuwasilisha kazi hizi kwa njia ya mtandao ni kuepuka malalamiko kuhusu watu wa kati au dhana ya Multichoice hutoa nafasi kwa kujuana.

“Uongozi wa Multichoice Tanzania unapenda kutoa pongezi kwa serikali kwa namna unavyotoa ushirikiano na kuweka mazingira rafiki na wezeshi ya kushirikiana.”alisema Shelukindo.

Akiendelea kuzungumza Bw.Shelukindo alisisitiza kuwa moja ya vitu vitakavyozingatiwa wakati wa uchambuzi maandiko hayo ni kuwepo kwa cheti cha umiliki wa ubunifu wa kazi hiyo kutoka COSOTA.
Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare (wa kwanza kulia) akifuatilia wasilisho la namna wadau wa tasnia ya filamu wanahitajika kuandaa andiko lao ambalo wataliwasilisha Multichoice kwa ajili ya kupata ufadhili wa fedha katika kuandaa kazi hiyo, kutoka kwa Mnufaika wa Mafunzo ya Uanadaaji wa Filamu kupitia Multichoice Bw.Wilson Nkya (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Multichoice Tanzania wa kutangaza fursa hiyo, katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo na wa kwanza kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano Multichoice Tanzania Bw.Ronald Shelukindo. Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo akiwasihi wadau wa tasnia ya filamu (hawapo pichani) kuchangamkia fursa iliyotolewa na Multichoice ya kutoa ufadhili wa uandaaji wa filamu leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza fursa hiyo.

Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo aliwasihi wadau wa tasnia ya filamu nchini kuacha malumbano, badala yake wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.

Vilevile Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Filamu Bw.Denis Sweya aliomba uongozi wa Multichoice kubadili lugha ya mikataba yao na kuwa kwa lugha ya Kiswahili ili wadau waweze kusaini wanachokielewa.

Katika kuhakikisha suala la tafsiri kwa lugha ya Kiswahili katika mikataba ya Multichoice linafanikiwa na kufanyiwa kazi kwa haraka COSOTA ilitoa ushirikiano kwa kuwasiliana na Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA, ambapo Multichoice waliridhia kuwasilisha nakala ya mkataba huo Machi 09, 2021 kwa ajili ya kuweza kutafsiriwa .

Halikadhalika Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Taifa Bw.Salum Mchoma alitoa ombi kwa uongozi wa Multichoice kutoa mafunzo kwa waigizaji ili waweze kufanya vyema katika kazi zao sababu wao ni watu wa mwisho katika mchakato wa uandaaji wa filamu ila ni watu muhimu katika kukamilisha kazi hiyo na kuonesha ubora wa kazi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news