AZIMIO LA BUNGE LA KUUTAMBUA NA KUUENZI MCHANGO WA RAIS WA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA UTUMISHI WAKE ULIOTUKUKA


AZIMIO LA BUNGE LA KUUTAMBUA NA KUUENZI MCHANGO WA RAIS WA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA UTUMISHI WAKE ULIOTUKUKA


(Kanuni ya 61 (1) ya Kanuni za Bunge Toleo la Juni, 2020)

_________________

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 61 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020, naomba kuwasilisha Hoja kwamba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Azimio la Kuutambua na Kuuenzi mchango wa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Utumishi wake uliotukuka;

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nichukue fursa hii kuwapa pole tena Watanzania na Waafrika kwa ujumla kwa kifo cha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021 Jijini Dar es Salaam. 

Hakika huu ni msiba mkubwa kwani tumempoteza kiongozi mchapakazi na mzalendo wa kwelialiyesimamia na kujenga Umoja wa Kitaifa, Uzalendo na Uadilifu;Mheshimiwa Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alishika rasmi madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05 Novemba, 2015. 

Katika kipindi chote cha uongozi wake alifanya kazi kwa bidii, umahiri, maarifa na kujitoa maisha yake kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Taifahili;Mheshimiwa Spika, ni wazi kwamba Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli kwa nchi yake. 

Mambo aliyoyafanya ni mengi kiasi kwamba kuyaorodhesha, kwa hakika itachukua miezi kadhaa kukamilika. Hata hivyo, katika kuutambua na kuuenzi mchango wa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, naomba nikumbushe machache ambayo aliyasimamia wakati wa uhai wake akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mheshimiwa Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliimarisha Utumishi wa Umma naMifumo ya Taasisi za Umma.

Katika hili alirejesha nidhamu na uwajibikaji miongoni mwa Watumishi wa Umma, hali ambayo imewezesha Wananchi kupata huduma bora na kwa wakati. 

Vilevile, aliimarisha maadili kwa viongozi wa umma kwa kuanzisha utaratibu wa Kiapo cha Uadilifu kwa Kiongozi wa Umma;Mheshimiwa Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuboresha huduma za jamii hususan kuboresha Elimu, Afya, Maji na Umeme Vijijini;

Kwa upande waelimu,alianzisha utaratibu wa elimu bila malipo kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Nne katika Mpango wa Elimu Msingi sambamba na kuongeza idadi ya Shule za Msingi kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi 17,804 mwaka 2020 na Shule za Sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi shule 5,330 mwaka 2020;

Kwa upande wa Afya, alifanikiwa kuwezeshakuongezwa kwa Bajeti ya kwa ajili ya ununuzi wa dawa kutoka Shilingi Bilioni 31 hadi kufikia zaidi ya Shilingi Bilioni 300, kuimarishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali za Rufaa kama vile MOI, Mloganzila na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Kuongeza Zahanati kutoka 6,044 hadi 7,242, Vituo vya Afya kutoka 718 hadi 1,205, kuajiri Watumishi kwa ajili ya kutoa huduma katika sekta hiyo na kuongeza upatikanaji wa dawa na Vifaa Tiba katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kote nchini;

Kwa upande wa sekta ya maji, pamoja na mambo mengine, alifanikiwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maji na hivyo kutimiza azma yake ya kumtua Mama ndoo kichwani. Aidha, alianzisha Taasisi ya RUWASA ambayoimekuwa kichocheo cha usambazaji na upatikanaji wa huduma za maji Vijijini na Mijini.

Kwa upande wa umeme, alifanikiwa kuimarisha hali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme hususan maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa kuongeza vijiji vilivyounganishwa na mpango wa umeme vijijini kutoka vijiji 2,018 mwaka 2016hadivijiji 10,312 Februari, 2021sawa na asilimia 84 ya idadi ya vijiji vyote nchini;

Mheshimiwa Spika, ametekeleza kwa vitendo uamuzi wa miaka mingi wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma,ambayo ilikuwa ni ndoto ya Rais wa Kwanza na Muasisi wa Taifa hili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970 sambamba na ujenzi wa Ofisi za Serikali na Taasisi za Umma. Jambo hili limerahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi nchi nzima na kuchochea ukuaji na ustawi wa Mikoa ya Kanda ya Kati;

Mheshimiwa Spika,kwa upande wa miundombinu,Serikali chini ya uongozi wa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imefanikiwa kuimarisha miundombinu katika nyanja zote ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamikama vile barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha. 

Aidha,aliwezesha ujenzi wa madaraja makubwa na barabara za juu (flyover na interchange),ujenzi wa barabara za By Pass Arusha na Mwanza, ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge)kutoka Dar es Salaam –Morogoro ambayo imekamilika na Morogoro –Dodomaambayo ujenzi wake umefikia takriban asilimia 50. Pamoja na hayo alifufua Shirika la Meli nchini kwa kununua Meli mpya Mwanza,kukarabati Meli ya MV Victoria,kujenga na kukarabati vivuko;

Vilevile, amefanikiwa kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka kuwa na ndege moja ndogo mbovu hadi kuwa na ndege kubwa kumi na moja hadi sasa. Aidha, alifanikiwa kuimarisha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara;Mheshimiwa Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alifanikiwa kutujenga Watanzania katika kujiamininakujinenea mema hadi tukaweza kuamini kuwa Tanzania sio nchi maskinibali nitajiri na inaweza kuwa miongoni mwa nchi wahisani (donor country);

Mheshimiwa Spika, katika sekta ya Viwanda,Uongozi wa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli uliweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda. 

Kutokana na mazingira hayo jumla ya viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa nchini kati ya mwaka 2015 na 2019. 

Kati ya viwanda hivyo 201 ni viwanda vikubwa, 460 viwanda vya kati, 3,406 viwanda vidogo na 4,410 viwanda vidogo sana. 

Katika juhudi za kuendeleza uchumi wa viwanda nchini aliweza,bila kuyumba,kusimamia uamuzi wakujengaBwawa la Nyerere ujenzi unaogharimu zaidi ya Trilioni 6 na utakaowezesha uzalishaji umeme wa Megawati 2,115;Mheshimiwa Spika, Mwezi Machi, 2020 ulipoibuka ugonjwa wa Corona, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alifanikiwa kutuondoa hofu Watanzania na kutujengea matumaini kwamba, tukimtanguliza Mungu mbele tutashinda mapambano dhidi ugonjwa huo. 

Aidha, alisisitiza kwamba pamoja na kuwapo kwa ugonjwa wa Corona ni lazima maisha yaendelee;

Vilevile alihimiza wananchi kutumia mbinu mbalimbali za kisayansi na za kiasili katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona,na alikataa kabisa kuiga mtindo wa kufunga mipaka ya nchi au kuwafungia wananchi wake wasitoke nje tofauti na viongozi wa mataifa mengine waliofunga mipaka ya nchi zao na kuzuia watu wao kutoka nje (lockdown). 

Msimamo huu una mchango mkubwa kwa Tanzania kupiga hatua kiuchumi kiasi cha kuingia uchumi wa kati;Mheshimiwa Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kinara wa kuikuza na kuitangaza Lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania. 

Kwa juhudi zake,Lugha ya Kiswahili imeweza kuingizwa miongoni mwa Lugha rasmi za SADC na pia nchi mbalimbali zimeingiza Lugha ya Kiswahili katika Mitaala ya Mataifa yao;Mheshimiwa Spika, mambo aliyofanya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ilikuwa ni kwa faida ya wanyonge nchini ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa hawanufaiki na rasilimali za nchi yao. 

Alikuwa mtetezi mkubwa wa makundi ya wananchi wa hali ya chini kama vile Machinga na Mamalishe. 

Naamini kila Mtanzania anajivunia namna Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alivyopigania na kujitolea maisha yake kwa faida ya nchi, kama ambavyo yeye mwenyewe siku za karibia na mwisho wa uhai wake alisema:...lakini ninajua Watanzania wananipenda, ninajua ninayoyafanya ni kwa maslahi mapana ya Watanzaniamaskini, kwa hiyo ndugu zangu tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kumtanguliza Mungu mbele kila mmoja kwa imani yake lakini tujenge Tanzania yetu. 

Mimi ni mtumishi wenu; na ninataka niwaambie ndugu zangu siku moja mtanikumbuka, na ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya, kwa sababu nime-sacrifice maisha yangu kwa ajili ya Watanzania masikini. 

Kwa kutokana na Miundombinu kutumika kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo;

KWA KUWA, kujiamini na kujinenea mema kiasi cha Watanzania kujitambua kama Taifa lao si maskini bali linaweza kuwa miongoni mwa nchi wahisani kumewezesha Taifa kuwa na ari ya kujitegemea katika ngazi ya maisha ya mtu mmoja mmoja na Taifakwa ujumla;

KWA KUWA, mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda yalichangia kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda na kuingia katika nchi zenye uchumi wa kati;

KWA KUWA,kukamilika kwa ujenzi wa Bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji kwa ajili ya uzalishaji umeme wa Megawati 2,115 kutaimarisha upatikanaji wa uhakika wa umeme na kwa bei nafuu na hivyo kwenda sambamba na Tanzania ya Viwanda jambo linaloendelea kukuza uchumi wa Taifa; 

KWA KUWA, kitendo cha kuwatoa hofu na kuwapa matumaini wananchi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Coronakwa kuwahimiza kumtanguliza Mungu, kutumia mbinu za kisayansi na kiasili katika kukabiliana na ugonjwa huona kukataa kuiga mtindo wa kufunga mipaka na kuwafungia wananchi wake wasitoke nje,kilizingatia hali halisi ya uwezo wa kiuchumi wa wananchi walio wengi ambao kipato chao ni cha chini kimeifanya nchi yetu isiyumbe kiuchumi na kuchangia kuingia kwenye uchumi wa kati; 

NA KWA KUWA, juhudi za Rais wa Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, katika kuikuza na kuitangaza Lugha ya Kiswahili nje na ndani na nje ya nchi kwa kutumia uhusiano wa kidplomasia kumewezesha Lugha hiyo kuingizwa kwenye Lugha rasmi za SADC na katika mitaala ya mataifa mbalimbali jambo litakalowezesha hata upatikanaji wa ajira;

KWA HIYO BASI,Bunge hili katika Mkutano wake wa Tatu, Kikao cha Kwanza, tarehe 30 Machi, 2021, linaazimia kwa dhati na kauli moja kwambatunautambua na tutauenzi mchango wa Rais waTanowa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa utendaji wake uliotukuka ambao umefanikisha kupunguza umasikini kwa wananchi,kuliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kati na kupandisha hadhi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,naomba kutoa hoja.Mhe. Najma Murtaza Giga, Mb.MBUNGE WA VITI MAALUM

30 Machi, 2021

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news