Mkutano wa Sita wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi wafunguliwa

Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Burundi umeanza rasmi mjini Kigoma, ukiwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutumia fursa zilizopo baina ya nchi hizo katika kukuza uchumi, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi unaofanyika mjini Kigoma kuanzia tarehe 3 hadi 5 Machi 2021. Mkutano huu umeanza kwa ngazi ya wataalam na utamalizika kwa ngazi ya Mawaziri tarehe 5 Machi 2021. Kulia walioketi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Isidore Ntirampeba.
Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi. 

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili masuala matano o ambayo ni pamoja na siasa na mahusiano ya kidiplomasia, ulinzi na usalama, maendeleo ya miundombinu, ushirikiano katika sekta ya uchumi na kijamii.

Alisema mafanikio ya mkutano huo yanategemea zaidi jitihada za pamoja kama watendaji katika kutekeleza masuala watakayokubaliana na kwamba kujadili kwa uhalisia na kufikia makubaliano yatakayotekelezeka ni moja ya lengo la mkutano huo.

“Katika mkutano huu tuwe tayari kusimamia na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa makubaliano na kuweka utaratibu wa kufanya mapitio ya utekelezaji wa masuala tutakayokubaliana angalau mara moja kwa mwaka,”alisema Balozi Ibuge.

Alisema kwa upande wa Tanzania utawekwa utaratibu wa kufanya mapitio ya mara kwa mara ya makubaliano yote yaliyofikiwa kwani kwa kufanya hivyo mkutano huo utatimiza matarajio ya viongozi wakuu na wananchi wa mataifa hayo mawili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Isidore Ntirampeba naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi unaofanyika mjini Kigoma.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko (kulia) akiwa na viongozi wengine kutoka Tanzania wanaoishiriki Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi ulioanza kufanyika kwa ngazi ya wataalam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Frank Mwega akizungumza kuhusu ratiba ya mkutano wa ngazi ya wataalam.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Burundi, Mhe. Isidore Ntirampeba alisema wanaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono ombi lao la kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuendelea kuwasemea kwenye majukwaa ya kimataifa ili waweze kuondolewa vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa na Jumuiya ya Ulaya.
Bw. Mwega akizungumza.
Sehemu ya ujumbe kutoka Burundi unaoshiriki mkutano wa wataalam wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Burundi.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Burundi.
Ujumbe wa Burundi.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wanaoshiriki mkutano sita wa tume ya pamoja ya kudumu kwa ngazi ya wataalam.
Ujumbe wa Tanzania.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa tume ya pamoja ya kudumu kati ya Tanzania na Burundi.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye mkutano.
Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa sita wa tume ya pamoja ya kudumu kati ya Tanzania na Burundi.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkutano.
Picha ya pamoja. 

“Tumejidhatiti kuhakikisha tunawaonesha wale wote wanaoiwekea vikwazo nchi ya Burundi kuwa wakati umeabadilika, kwani sasa tunayo amani na utulivu na kwamba tupo kwenye juhudi kubwa za kuimarisha ushirikiano na nchi zote na washirika wa maendeleo wenye mapenzi mema na nchi yetu,”alisema Ntirampeba.

Mkutano huo ambao umefunguliwa leo kwa ngazi ya wataalam utafuatiwa na Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Mambo ya Nje za Burundi na Tanzania ambao wanatarajiwa kusaini makubaliano yaliyofikiwa na pande zote mbili kwa ajili ya utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments