BREAKING NEWS: Rais Samia amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bandari nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasaan ameagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini,Mhandisi Deusdedit Kakoko huku uchunguzi ukiendelea baada ya kubainika ubadhirifu mkubwa wa fedha sh.Billioni 3.6, pia amemuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU kuanza uchunguzi ma ramoja, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Uamuzi huo ameuchukua leo, baada ya kupokea taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20 na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020.

Pia ameelekeza kuwa, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iwajibishwe kwa sababu inachukukua pesa nyingi huku matokeo yakiwa hayaonekani.

Rais Samia amesema, ndani ya TAMISEMI kuna ufisadi mkubwa ambapo ameagiza CAG achunguzwe akishindwa aseme Serikali ifanye kazi.

Pia ametoa maagizo kuwa, mashirika ya umma yachunguzwe kwa sababu katika takwimu za ufisadi mashirika ya umma yanaongoza kwa ubadhirifu na Serikali ipo tayari kufanya maamuzi kama CAG atashindwa.

Awali, CAG amesema kati ya hati 900 alizozikagua, hati 800 sawa na asilimia 87 zinaridhisha huku hati 81 zikiwa na mashaka na mbaya ni 10.

CAG Kichere ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti aliyoifanya kwa taasisi za Serikali Kuu, mamlaka ya serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na vyama vya siasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ulioishia Juni 30, 2020.

“Tumeongeza mashirika 10 ambayo tunayakagua na nimeshirikiana na makampuni mengine binafsi kuhakikisha tunakagua ipasavyo pia tumefanya kaguzi za kitaalamu SGR, miundombinu mabasi yaendayo haraka, barabara kuu Morogoro, Kibaha, miradi ya maji wilaya ya Same na Korogwe,” amesema CAG.

Pia CAG amesema , mwenendo wa hati za ukaguzi na tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika ukaguzi mwaka 2019/2020, ametoa jumla ya hati  900 za ukaguzi.

“Hati 243 za Serikali Kuu 235 zinaridhisha na nyingine sita zina mashaka, mamlaka ya Serikali za mitaa ni  185 na kati ya hizo 124 zinaridhisha na zenye mashaka 53 na zilizokutwa ni mbaya ni nane.Mashirika ya umma nimetoa hati 165 na kati yake 162 zinaridhisha na zenye mashaka ni tatu. 290 ni hati za miradi ya maendeleo na kati ya hizo 275 zinaridhisha na zenye mashaka ni 15 na hapa hakuna hati mbaya,” amesema.

Amesema, alikagua hati 17 za vyama vya siasa kati ya hizo nne zinaridhishana zenye mashaka ni nne, ambapo kati yake, ameshindwa kutoa maoni kutokana na mambo mbalimbali.

“Jumla kuu ya hati zenye mashaka ni 81, sawa na asilimia tisa na hati mbaya ni 10 sawa na asilimia moja na hati 90, nimeshindwa kutoa maoni sawa na asilimia moja,”ameongeza CAG.

Post a Comment

0 Comments