BREAKING NEWS:Aliyekuwa bosi wa Bandari Mhandisi Kakoko akamatwa

Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan yameanza kufanyiwa kazi baada ya ndani ya siku moja mamlaka husika kuchukua hatua kwa kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Mhandisi Deusdedit Kakoko, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Ni baada ya Rais Samia, Machi 28, mwaka huu kumsimamishwa kazi Mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubadhirifu zinazoikabili mamlaka hiyo.

Rais Samia alifanya maamuzi haya baada ya kupokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2019/2020 ambayo imeonesha ubadhirifu mkubwa bandarini.
 
“Kuna ubadhirifu mkubwa Bandarini naomba TAKUKURU ikafanye kazi, nimeletewa ripoti ya ubadhirifu wa Bilioni 3.6. Imani yangu ni kwamba ndani ya Shirika la Bandari kuna ubadhirifu kama wa sh. Bilioni 3.6, lakini Waziri Mkuu amefanya ukaguzi na waliosimamishwa ni wa chini, nimeomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu uchunguzi uendelee,”amesema.

Habari zilizoifikia DIRAMAKINI zimeeleza kuwa, Mhandisi Kakoko baada ya agizo la Rais makachero wa Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake mkoani Dar es Salaam na kukuta kiasi kikubwa cha fedha, hivyo kukamatwa kwa hatua zaidi.

"Ndiyo, kuna kiasi kikubwa cha fedha ambazo zimekamatwa nyumbani kwake baada ya uchunguzi, zikiwa katika mafungu ya dola za Kimarekani, bila shaka muda ukifika vyombo husika vitatoa taarifa kamili kwa umma, Rais akitoa maagizo lazima yafanyiwe kazi mara moja kwa hatua za haraka,"chanzo cha taarifa kimeidokeza DIRAMAKINI kwa sharti la kutoandikwa jina lake.
 
Taarifa zaidi tutaendelea kukupasha kupitia hapa, endelea kufuatilia DIRAMAKINI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news