BRELA YAPONGEZWA KWA KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe ameipongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuwafikia wajasiriamali na kuwapa elimu pamoja na hamasa ya kurasimisha biashara zao.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe akisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA alipotembelea banda hilo lililopo katika maonesho ya Viwanda vya Wanawake yanayoendelea katika viwanja vya Posta Kikitonyama jijini Dar es Salaam.

Waziri Kigahe ameyasema hayo Februari 27, 2021 katika uzinduzi wa Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonesho ya Bidhaa katika Viwanja vya Posta/TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam.

"Pamoja na kazi nzuri mnayoendelea kuifanya kama taasisi, nimefurahishwa sana na uwepo wenu katika maonesho haya, hapa mnawafikia Wajasiriamali kwa pamoja na kuwapa elimu kuhusu urasimishaji wa biashara na faida zake katika kukuza uchumi wa taifa,"an\mesema Mhe. Kigahe.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa akizungumza na waandishi wa habari amebainisha kwamba, Dira ya BRELA hivi sasa ni kuwafikia Wadau wake katika maeneo yao na kuwapa elimu kuhusu urasimishaji biashata pamoja na huduma za papo kwa hapo inapowezekana.

"BRELA ya sasa sio kama ya zamani, tumefanya maboresho makubwa mpaka sasa na bado tunakuja na mikakati mikubwa na bora kabisa ya kuhakikisha tunawafikia wadau wetu katika mashina yao.
Ushiriki wetu katika maonesho kama haya ni njia moja lakini kuna mikakati mingine kama kuandaa warsha na semina nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu na hamasa ya urasimishaji biashara,"amesema Bw. Nyaisa.

Katika hatua nyingine, Bw. Nyaisa ameomba Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) zikae kwa pamoja na kupata muafaka kuhusu namna ya kuwatumia Maafisa Biashara ili kutokana na Urasimu unaojitokeza na mfumo dhaifu wa utoaji huduma kwa wadau pindi wanapofanya sajili katika Halmashauri zao.

Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonesho ya Bidhaa yalizinduliwa yalizinduliwa Februari 27,2021 na yanatarajia kufikia hitimisho machi 6, 2021.

Post a Comment

0 Comments