DIRAMAKINI TUNAUNGANA NA WATANZANIA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAOMBOLEZO

Menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa www.diramakini umesikitishwa na kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.
Tunaungana na wote kwa dua na sala ili mpendwa wetu apumzike kwa amani. Mungu amlaze mzee wetu mahali pema.

Ni ombi letu kwa Watanzania, katika kipindi hiki kigumu yatasemwa mengi kwa sababu Taifa letu linazungukwa na maadui wengi wa ndani na nje kuliko watu wema, hivyo tusikubali kugawanywa, tuendelee kudumisha umoja, mshikamano na amani ya Taifa letu.

Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji
Diramakini Business Limited
Machi 18, 2021.

SPIKA AUNGANA NA WATANZANIA

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai amesema kuwa kufuatia kifo cha Rais  Watanzania wanakazi yakuhakikisha wanaendeleza yale ambayo Rais Magufuli alikuwa akiyafanya katika kipindi cha uhai wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai alisema kuwa Rais alikua mjenga Nchi hasa katika swala zima la miundombinu na  miradi mikubwa mingi kama elimu, afya na barabara nakusema kuwa Rais ameacha alama katika kila nyanja.

"Mh.Rais wetu mpendwa John Magufuli alikuwa ni mpenda maendeleo na katika uhai wake amegusa katika kila nyanja hakika kaacha alama nakutuachia majonzi makubwa watanzania,"amesema Ndugai.

Amesema kuwa kazi zote alizokuwa akizifanya Rais, hotuba alizozitoa bungeni sambamba na utekelezaji wa ilani ya  chama cha mapinduzi ya mwaka 2025 zitasimamiwa na kutekelezwa kwa kuongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassani.

Aidha, ameagiza Wabunge wote waliokuwa kuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya  maendeleo warudi haraka na mpaka sasa wabunge wote wako njiani kurudi dodoma.

Sambamba na hayo amesema kuwa Rais alikuwa muhimili wa pili wa Bunge hivyo ni pigo kwa Bunge na amemuachia kazi kubwa mama samia na viongozi wote na serikali kwa ujumla  huku akitoa pole kwa mama Janeth mke wa marehemu, familia ya marehemu na watu wa Chato na kwa Watanzania wote.

Post a Comment

0 Comments