Hawa ndiyo Marais walioiongoza Tanzania tangu Uhuru hadi leo

Tangu Uhuru, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kijamii, kitamaduni na kiuchumi.

Hayo ni matunda ya uongozi mahiri na shupavu kutoka kwa Marais waliongoza katika nchi ya Tanzania kwa nyakati tofauti ambao wameleta maendeleo makubwa katika taifa na mchango wao utaendelea kukumbukwa vizazi na vizazi.

Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndie aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania na alifuatiwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi, mwaka 1985.

Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania na alifuatiwa na Hayati Benjamin William Mkapa, mwaka 1995.

Hayati Benjamin William Mkapa, alikuwa Rais wa Tatu wa Tanzania na alifuatiwa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Awamu ya Nne mwaka 2005.

DK. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Rais wa nne wa Tanzania na alifuatiwa na DK. John Pombe Joseph Magufuli, mwaka 2015.

Baadaye alikuja Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa Rais wa Awanu ya Tano wa Tanzania akifuatiwa na Samia Suluhu Hassan,mwaka 2021.

Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita wa Tanzania ambaye pia ni Mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika ukanda wa Africa Mashariki.

Post a Comment

0 Comments