🔴𝐋𝐈𝐕𝐄: Ibada ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli

Kutokea Kanisa la St.Peters Dar es salaam, mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dr.John Pombe Magufuli tayari umefikishwa kwa ajili ya Ibada kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili kuagwa.

KUTOKA KANISANI
RAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI, MABALOZI MBALIMBALI KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaongoza viongozi waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwemo Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli huku baadhi ya mabalozi wakibubujikwa na machozi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan amesaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Kamrijee Dar es Salaam mchana wa Machi 19, 2021 na kufuatiiwa na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena kwa maradhi ya moyo.

Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Hussein Ally Mwinyi nae pia amesaini kitabu cha maombolezo akifuatiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othaman Masoud

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini walishindwa kujizuia na kutokwa na machozi kumlilia Hayati Dkt. Magufuli na kumuelezea kuwa alikuwa kiongozi jasiri na mzalendo si kwa manufaa ya Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla ambapo Balozi wa Jamaica hapa nchini Mhe. Velisa Delfosse amemuelezea Hayati Dkt Magufuli kama mwanampinduzi na mzalendo halisi wa Afrika wa wakati huu.

“Rais Magufuli alikuwa mwanampinduzi na mzalendo halisi wa Afrika wa wakati huu, kwa kweli tumeguswa sana na msiba wake hakika pengo lake halitazibika, tunamuombea kwa Mungu apumzike salama,”amesema Balozi Delfosse.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Othman Masoud akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Nae Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Wang Ke mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo amemuelezea Hayati Magufuli kama kiongozi mwenye maono na mzalendo mwaminifu kwa Afrika,na kwamba atakumbukwa na Watanzania kwa jitihada zake kubwa za kuleta mabadiliko chanya ili kuinua hali ya maisha hususani wale wa kipato cha chini.

Kwa upande wake Balozi wa Sudani ya Kusini Mhe. William Ruben amewasihi viongozi wa Afrika na Watanzania kwa ujumla kufuata nyayo za Hayati Dkt Magufuli kwa kuwa alikuwa alama halisi ya Afrika na alitufundisha wengi wetu kuamini kuwa Afrika imebarikiwa na ni tajiri kinyume na tulivyoamini kuwa tunahitaji msaada kutoka kwa mataifa ya nje ya bara la Afrika

“Naomba kuwasihi viongozi wa Afrika na Watanzania kwa ujumla kufuata nyayo za Hayati Dkt Magufuli kwa kuwa alikuwa alama halisi ya Afrika na alitufundisha wengi wetu kuamini kuwa Afrika imebarikiwa na ni tajiri kinyume na tulivyoamini kuwa tunahitaji msaada kutoka kwa mataifa ya nje ya bara la Afrika,”amesema Balozi Ruben.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.



Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Benson Chali akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Mary O’neill kisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN), Zlatan Milisic akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Balozi wa Hispania, Mhe Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Balozi wa Rwanda Meja Jenerali Charles Karamba akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
 
Mabalozi wengine waliofika katika viwanja vya Karimjee na kusaini kitabu cha maombolezo ni pamoja na Balozi wa Morocco Mhe. Abdililah Benryane, Balozi wa Ethiopia Mhe Yonas Sanbe, Balozi wa Qatar Mhe Abdulla Jassim Al Madadadi, Balozi wa Japan Mhe Shinichi Goto Balozi wa Palestina Mhe Derar Ghannan, Balozi wa Cuba Mhe Lucas Damingo, Balozi wa Pakistan Mhe Mohammed Salem, Balozi wa Uswis Mhe Didier Chassot, Balozi wa Ireland Mhe Mary Oneill.

Wengine ni Balozi wa Rwanda Meja Jeneral Charles Karamba, Balozi wa Syria Dr Sawsan Alani, Balozi wa Korea Mhe Kim Yong Su, Balozi wa Iran Mhe Hussein Alvandi Behined, Balozi Hispania Mhe Fransisca Pedros, Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Chali na Balozi Vietnam Mhe Nguyen Namtien.

Baadhi ya Wakuu wa mashirika na Taasisi za Kimataifa waliofika kusaini kitabu cha maombolezo ni pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Mhe. Zlatan Milisic, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF, Mhe. Shahini Bahuguna,Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni Mhe Tirso Do Santos,Shirika la Kazi duniani Wellingtone Chibebe,Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa Mhe Christine Musisi na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Mhe Antonio Jose Canandula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news