Juma Duni Haji: Tanzania imempoteza shujaa, ACT Wazalendo tunatoa pole

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ni pigo kubwa katika taifa na kuwataka Watanzania wote kuwa wavumilivu kipindi chote cha msiba, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji akisaini kitabu cha maombolezo.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Duni Haji aliyasema hayo akiwa katika Ofisi Kuu ya CCM iliyopo Kiswandui jijini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa viongozi wa CCM na Watanzania kwa kuondokewa na kiongozi huyo.

Amesema, kuondokewa na mwenyekiti na akiwa Rais ni jambo zito sana na kusema inahitajika uwepo wa subra miongoni mwa Watanzania na familia na wana CCM kwa ujumla.

Amesema kuwa, Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alikuwa Rais aliyesimama katika majukwaa na kusema wazi wazi kuwa anayaunga mkono na ataendeleza maridhiano.

“Sasa ni wajibu wetu sisi tulio hai kuyaendeza na kuyaenzi ili walioazisha ambao wameshatangulia mbele ya haki tuwatendee haki,”amesema Haji.

Duni amesema, viongozi wa CCM jinsi walivyowapokea inaonyesha ni kiasi gani yale maridhiao yaliosisiwa na marehemu Malim Seif Sharif Hamad pamoja na baadhi viongozi wa CCM yanaenendelezwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Amesema kuwa, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi alipofariki aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo walifika ofisini kwao Vuga kutoa mkono wa pole.

“Kwa hali hiyo uaona ni kiasi gani maridhiano yanaendelezwa na tumeaambiana kuwa Wazanzibar na watanzania kwa jumla sisi ni wamoja tuendeleze umoja wetu,”amesema Duni.

Amesema kuwa,kwa niaba ya chama cha ACT Wazalendo anatoa pole kwa Rais mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kutoa polea kwa wanachama wote wa CCM kuondokewa na mwenyekiti wao ambapo ni pigo kubwa kwa Taifa.

Haji alieleza kuwa, Wazanzibar ni wamoja na hapana budi kushirikiana hasa katika matukio haya ya misiba ambayo yameshawahi kutokea.

Hata hivyo amesema matukio kama hayo huwa sababu nyingine ya kuwaunganisha Wazanzibar na kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na huungana pamoja kata kujega taifa.

“Hakuna mtu aliyetegemea kama matukio hayo ya kifo yatatokea, lakini kazi ya mumba haina makosa,” amesema Haji.

Kwa upande mwingine alisema kuwa, marais waliopo sasa wote ni wapya na wanategemea kuwa na siasa za umoja na ushirikiano kwa maslahi mapana ya taifa.

“Tunampongeza mama Samia kwa kuchukua dhamana kubwa na tunategemea kuwa na siasa za maridhiano katika ardhi ya Tanzania,”amesema.

Sambamba na hilo amewataka watanzania kushirikiana pamoja katika kusitiri kiongozi huyo ambaye alifariki Machi 17, mwaka huu wakati akiwa katika matibabu katika Hospitali ya Mzena iliyopo mkoani Dar es Salaam.

Awali uongozi wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Makamu huyo walifika Wizara ya Habari Zanzibar na kuweka saini zao katika kitabu cha maombolezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news