Machi 28 ngumu; Wakurugenzi nane kikaangoni kufuatia agizo la Rais Samia


Wakurugenzi nane ambao Halmashauri zao zimepata Hati Chafu majina yao kuwasilishwa katika Mamlaka ya Uteuzi kwa hatua zaidi,anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Akizungumza na Waandishi wa habari Habari Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, amesema atawasilisha majina ya Wakurugenzi hao kwenye Mamlaka yao Uteuzi kwa ajili ya hatua stahiki.
 
"Kwakuwa Wakurugenzi wa Halmashauri Mamlaka yao ya Uteuzi ni Mhe. Rais, nitawasilisha majina yao ili wachukuliwe hatua kwa kadiri atakavyoona inafaa‘ amesema Jafo.

Wakati huo huo Waziri Jafo amewataka watendaji wote katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu katika kuwatumikia wananchi.

Post a Comment

0 Comments