Mama Samia awasilisha salamu za Rais Magufuli kwa Watanzania

"Nimekuja hapa (Tanga) niwasalimie, lakini kubwa niwape salamu za Rais, Rais anawasalimia sana na anawashukuru sana kwa kazi nzuri mliyofanya mwaka jana kurudisha Serikali ya CCM madarakani, Rais anasema tupo salama, tuchape kazi, twende vizuri,tujenge upendo na mshikamano wa Watanzania ili Taifa letu likuwe, liwe na tija zaidi; ... ANARIPOTI Mwandishi Diramakini (Tanga).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Handeni Mkoani Tanga leo March 15,2021, Makamu wa Rais ameanza ziara ya kikazi ya siku 5 Mkoani Tanga kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Wananchi. kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shegela na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Mhe. Henri Shekifu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo Machi 15, 2021 baada ya kuanza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Pia amewataka Watanzania kuacha kusikiliza maneno yanayozua taharuki na kuvuruga mshikamano na badala yake washirikiane ili kudumisha amani ya nchi iliyopo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu Mipango endelezi ya Kiwanda cha Kuchakata Mahindi Michungwani Segera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga kutoka kwa Meneja Mtendaji wa Kiwanda hicho John CK leo March 15,2021, Makamu wa Rais ameanza ziara ya kikazi ya siku 5 Mkoani Tanga kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Wananchi. kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shigela.  

Makamu wa Rais amesema, kwa sasa kumeibuka maneno mengi ambayo asilimia kubwa yanatoka nje hivyo aliwahakikishia Watanzania kuwa wako salama kubwa zaidi waendelee kushikamana na kudumisha amani ya nchi iliyopo.

"Kama mnavyojua hivi sasa maneno ni mengi, ni mengi mno nataka kuwahakikishia kwamba mpo salama, hivyo Watanzania tushikamane, tushirikiane wote tusimame kama watanzania kuijenga nchi yetu,"amesistiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mkata Wilayani Handeni Mkoani Tanga, leo March 15,2021, Makamu wa Rais ameanza ziara ya kikazi ya siku 5 Mkoani Tanga kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Wananchi. 

Ameongeza kuwa, maneno hayo mengi mengine hayatoki ndani yanatoka nje, "hivyo wapuuzeni endeleeni kufanya dua zenu, lakini tushirikiane, tushikamane, twende na Tanzania yetu tupo salama,"amesema.

Aidha, Mama Samia alisema madhumuni makubwa ya kufanya ziara mkoani Tanga ni kupita na kuangalia, shughuli za maendeleo zinazoendelea hasa katika majengo ya utawala, miradi ya maji, afya na miradi mingine inayotekelezwa na kujua namna ya kutatua changamoto ili miradi iweze kuendelea.
 
Naye Mkuu wa Mkoa Tanga, Martine Shigela amesema wamepokea sh.bilioni 7.2 kwa ajili ya miradi ya majengo matatu ya halmashauri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe Kuweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Kuchakata Mahindi Michungwani Segera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo March 15,2021, Makamu wa Rais ameanza ziara ya kikazi ya siku 5 Mkoani Tanga kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Wananchi. kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shigela.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimwagilia Maji Mti aina ya Paukaria alioupanda katika eneo la Kiwanda cha Kuchakata Mahindi Michungwani Segera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo March 15,2021 baada ya kuweka Jiwe la Msingi Kiwanda hicho. Makamu wa Rais ameanza ziara ya kikazi ya siku 5 Mkoani Tanga kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Wananchi. kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shegela.

Majengo hayo ni pamoja na Handeni Mji, Handeni Vijijini pamoja na Bumbuli ambapo yatasaidia kuondoa changamoto ya utendaji kazi kwa watumishi waliokuwa wanakumbana nayo hapo awali.

"Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imetoa kiasi cha shilingi bilioni 7.2 kwa ajili ya halmashauri hizo tatu ambapo Halmashauri ya Bumbuli imegharimu bilioni 2.5, Handeni Mji 2.7 na Handeni Vijijini bilioni 3.3,"amesisitiza Shigela.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo hilo la Halmashauri ya Handeni vijijini Mhandisi wa mradi wa jengo hilo la Halmashauri ya Handeni Vijijini, Henry Mshahara alisema kuwa, hadi kukamilika kwa jengo hilo kiasi cha shilingi bilioni 5.3 zitagharimu hadi kukamilika kwa jengo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news