Nabii Joshua ataongoza Siku Maalumu kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Dkt.Magufuli, kumuombea Rais Samia


Kongamano la Pasaka 4/4/2021 litaambatana na ibada ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, na kumuombea Mama yetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ili Mungu amuongoze katika kuliongoza Taifa letu kwa mafanikio makubwa. Ibada hiyo itafanyika katika makao makuu ya Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania (KWA NABII JOSHUA) yaliyopo Yespa, Kihonda mjini Morogoro.

Post a Comment

0 Comments