Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi asaidia kufuma makuti ya kuezeka soko la wanawake wajasiriamali


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini, Khamis Hamza Chilo akimsaidia kufuma makuti mmoja wa wananchi (hayupo pichani), ambapo makuti hayo yatatumika kuezekea soko dogo la kinamama wajasiriamali wa Shehia ya Kidimni, wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Mwananchi wa Kijiji cha Kidimni, Aviwa Khamis Muhammad akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini,Khamis Hamza Chilo(kushoto) huku wakifuma makuti kwa ajili ya kuezekea soko dogo la kinamama wajasiriamali wa Shehia ya Kidimni,wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini, Khamis Hamza Chilo akizungumza na mwananchi wa Kijiji cha Kidimni, Aviwa Khamis Muhammad (kulia) huku akimsaidia kufuma makuti kwa ajili ya kuezekea soko dogo la kinamama wajasiriamali wa Shehia ya Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Post a Comment

0 Comments