Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja akagua miradi ya utalii Geita

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Mkoa wa Geita ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya kiutalii inayotekelezwa na taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mkoani humo, anaripoti John Bera (WMU) Geita.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo wakati wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo.

Akiwa katika ziara hiyo amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa na wale wa taasisi zilizo chini ya wizara kuhusu namna bora ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

Amesema, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa vizuri litaongeza mapato.

"Tuhamasishe zao la asali linalotokana na nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao Serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia pato la Taifa,"amesema Mhe.Mary.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news