NEC yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma baada ya kupokea Barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari jijini Dodoma Machi 27, 2021, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera amesema uchaguzi huo umeapangwa kufanyika tarehe 2 Mei,2021.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya kiti cha Ubunge katika Jimbo la Muhambwe, Halmashauri ya Wilaya
ya Kibondo, Mkoani Kigoma,”amesema Dkt.Mahera.

Aidha, kwa kuzingatia kifungu cha 37 (1) (b), cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinaitaka Tume kujaza nafasi ya kiti cha Ubunge katika kipindi kisichopungua siku 20 na kisichozidi
siku 50 tangu kutokea kwa sababu iliyoacha nafasi wazi ya kiti hicho.

“Kutokana na matakwa hayo ya kisheria, Tume inautaarifu Umma kuwa Jimbo la Muhambwe liko wazi na uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 3 Aprili, 2021 Hivyo, uchaguzi ambayo ni siku ya 49 tangu
kutokea kwa kifo hicho,”amesema Dkt. Mahera.

Amesema kuwa maandalizi kwaajili ya uchaguzi huo yameshafanyika na kazi ya utoaji fomu za uchaguzi kwa wagombea inaanza 28 Machi hadi 3 Aprili, 2021 huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hiyo ukifanyika 3 Aprili mwaka huu.

Aidha Dkt.Mahera amesema, kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo zitaanza 3 Aprili 2021 na zitafikia ukomo wake Mei mosi mwaka huu na uchaguzi kufanyika 2 Mei,2021.

Mahera amesema tayari Tume imekwisha vitaarifu Vyama vya Siasa kwa njia ya barua juu ya kuwepo kqwa uchaguzi huo mdogo na inavikumbusha kuzingatia sharia, kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Miongozo na Maelekezo ya Tume wakati wote wa kipindi cha Uchaguzi.

Pia Mahera ametumia fursa hiyo kutoa salamu za pole kwa viongozi wa Serikali, Familia na Watanzania wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

“Tume inatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Familia ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Chama cha Mapinduzi na watanzania wote kwa ujumla,” amesema Dkt. Mahera.

Uchaguzi katika jimbo la Muhambwe unafanyika baada ya Mbunge wa Muhambwe (CCM) mkoani Kigoma Atashasta Justus Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 ambaye alifariki akiwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari
eneo la Nanenane jijini humo Februari 11, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news