“Nimeona nisimame hapa niwasalimu ndugu zangu"-----Hakika tutakukumbuka Baba yetu Hayati Dkt.John Magufuli

-Hii kauli wananchi waliizoea kuisikia kutoka kwako kila unapopita.

-Leo mioyo yao imepatwa ganzi na simanzi na kujiuliza, why unapita kimya kimya?.

-Wananchi hawa wanyonge hawajaacha desturi uliyowazoesha ya kusimama pembeni ya barabara kukulaki na kukusimamisha, lakini leo wanahuzuni kwani shida na kero zao huzisikii tena.

_Hawakuoni juu ya gari tena kama walivyozoea.

_Nenda JPM uliyekuwa kipenzi cha Watanzania.

-Rais asiyekuwa na makuu, alijishusha na kuyaishi mazingira ya Watanzania wote bila kujali mwenye nacho au asiyenacho. Hakika tutakuenzi daima Baba yetu mpendwa.

Post a Comment

0 Comments