Rais Dkt.Mwinyi amuapisha mrithi wa Maalim Seif, Makamu wa Kwanza wa Rais

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kufuatia uteuzi alioufanya jana Machi 1, 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo Machi 2,2021.

Uteuzi wa Othman Masoud Othman unafuatia kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia Februari 17, mwaka huu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe.Othman Masoud Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zuberi Ali Maulid na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masod Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa iliofanyika leo, katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.Hafla hiyo ya kiapo ilifanyika jana Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaab na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid.

Wengine ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Juma Abdalla Sadalla, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zubeir Zito Kabwe, mawaziri, wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini pamoja na wanafamilia.

Rais Dkt.Mwinyi amemuapisha kiongozi huyo kushika wadhifa huo kutokana na matakwa ya Kikatiba chini ya kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kilichobainisha kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi alimteua kiongozi huyo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 baada ya kushauriana na Chama cha ACT Wazalendo.
Kabla ya uteuzi huo Othman Masoud Othman aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwemo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Katika hatua nyingine, akizungumza na vyombo vya habari, Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman alisema atatumia uzoefu mkubwa alionao kumsaidia Rais wa Zanzibar kujenga na kuendeleza misingi ya maridhiano ya umoja wa kitaifa kwa maslahi mapana ya Wazanzibar. Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Viongozi wa Dini wakifuatilia kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Othman Masoud Othman, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisaini hati ya kiapo baada ya kumalizika kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha na pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliosimama nyuma na waliokaa kutoka (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha na pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa waliosimama nyuma na waliokaa kutoka (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman,baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapisha iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, baada ya kumalizika kwa kuapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Pichazote  na Ikulu).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar akisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo 2-3-2021.Ikulu Zanzibar.

Amesema, atasaidia kuimarisha misingi ya sera katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutengeneza sera bora ili kuleta maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusimamia ustawi mwema wa wananchi.

Aidha, amesema atasaidia kujenga Serikali itakayoweza kusimamia maridhiano ya nchi ili kuendeleza amani na umoja uliopo, akibainisha kuwa yeye ni muumini wa kushajiisha umoja miongoni mwa Wazanzibari.

Vile vile amesema, atatumia uzoefu mkubwa alionao Kimataifa katika kusimamia misingi ya rasilimali za Serikali, uwekezaji pamoja na uwajibikaji katika taasisi za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news