Rais Dkt.Mwinyi asaini vitabu vya maombolezo kifo cha Hayati Dkt.Magufuli

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesaini vitabu vya maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kueleza kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye alikuwa kipenzi cha watu, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kusaini Kitabu cha maombolezi ya kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,(Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Mwinyi kwa nyakati tofauti leo Machi 24, 2021 ametia saini vitabu hivyo ambapo alianzia katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar iliopo Kisiwandui jijini Zanzibar na kusaini kitabu cha maombolezo.

Akiwa katika ofisi hizo za CCM Zanzibar, Rais Dkt.Mwinyi amewakaribisha wale wote walioguswa na msiba huo kwenda kusaini kitabu hicho cha maombolezo hapo katika Ofisi Kuu ya CCM, iliopo Kisiwandui jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, baada ya kumaliza kusaini Kitabu cha maombolezi ya Kifo cha Hayati Dkt.John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.(Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Hussein Mwinyi ameeleza kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt.John Pombe Magufuli na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu kuilaza roho ya marehemu mahali pema peponi.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt.John Pombe Magufuli. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amin,”amesema Dkt.Mwinyi.

Rais Dkt. Mwinyi pia, alimuelezea Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli kwamba alikuwa kipenzi cha watu huku akitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kujitokeza kwa wingi Machi 23.2021 katika kuuaga mwili wa Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini Kitabu cha maombolezi ya Kifo cha Hayati Dkt.John Pombe Magufuli, alipofika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar leo 24-3-2021.(Picha na Ikulu).

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi aliwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba waridhike na wale wachache ambao watapata fursa ya kwenda kuuzika mwili wa mpendwa wao Marehemu Dkt. John Magufuli kijijini kwao Chato Machi 26, mwaka huu ambao watafanya hivyo kwa niaba yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini Kitabu cha maombelezi ya Kifo cha Hayati Dkt.John Pombe Maguful, aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alipofika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Ameongeza kwamba, anafahamu kuwa wananchi wote wa Zanzibar wangependelea kushiriki kikamilifu katika mazishi hayo ya mpendwa wao huko Chato, lakini kutokana na hali na mazingira yaliopo waridhike na uwakilishi uliopo ambao umeweza kuwakilisha vyema tokea kuanza kuagwa mwili huo huko jijini Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza hadi kuelekea kule Chato.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amefika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil ulioko Kikwajuni jijini Zanzibar na kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

Post a Comment

0 Comments