Rais Dkt.Mwinyi awaapisha mawaziri watatu,Kamishna wa Bodi ya Mapato

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mawaziri watatu aliowateua Machi 3, mwaka huu, kushika nyadhifa katika wizara tofauti za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
Wimbo wa Taifa.

Mawaziri walioapishwa ni Dkt.Sada Mkuya Salum anayekuwa Waziri katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Nassor Ahmeid Mazrui (Wizara Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto) pamoja na Omar Said Shaaban atakayeiongoza Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

Uteuzi wa Mawaziri hao unakamilisha idadi ya Mawaziri 16 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya Wizara hizo (tatu) kuwa wazi tangu pale Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alipotangaza Baraza la Mawaziri kwa mara ya kwanza Novemba 19, 2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri na Kamishna wa ZRB katika ukumbi wa Ikulu walioteuliwa hivi.
Viongozi wa Serikali na Mawaziri Wateuli wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbi wa Taifa na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapisha, (kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Dkt, Mwinyi Talib Haji.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemuapisha Salum Yussuf Ali kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) baada ya kumteua February 10, 2021.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa, akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid.

Wengine ni pamoja na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Mawaziri, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Vyama vya Saisa pamoja na wanafamilia.

Rais Dk. Mwinyi amewaapisha Viongozi hao kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifunguvya 42, 43 (1) (2) na 44 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka1984.

Katika hatua nyengine, wakizungumza na vyombo vya habari, Mawaziri hao wamesema wamejipanga kumsaidia Rais Dk. Mwinyi ili kukidhi matarajio makubwa waliyonayo Wazanzibari katika kupata maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo 4-3-2021 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Nassor Ahmed Mazrui kuwa Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-3-2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, baada ya kumaliza kula kiapo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Omar Said Shaaban, kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu).

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Sada Mkuya Salum alisema atahakikisha utekelezaji wa sera ya uchumi unafanyika kuambatana na usimamizi mzuri wa mazingira yaliopo.

Aidha, amesema atahakikisha sera ana sheria zote zitakazotungwa na kutekelezwa znchini inazingatia masuala yote mtambuka.

Nae, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban alisema atafanya kila juhudi kuhakikisha Zanzibar inarejea katika hadhi yake ya kuwa kitovu cha Biashara katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Amesema, ili kufanikisha azma ya Uchumi wa Buluu, atahakikisha Zanzibar inanufaika na malighafi zote za bahari.

“Chini ya usimamizi wa Rais, tumejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi,”amesema Waziri wa Afya ,Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto Nassor Ahmeid Mazrui.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news