Rais Kenyatta azifungia kaunti tano kwa kubainika na maambukizi makubwa ya Corona

Serikali ya Jamhuri ya Kenya imezifunga kaunti tano ikiwemo ya Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19), anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Nairobi).

Uamuzi huo umefanywa na Rais Uhuru Kenyatta ambapo amesema,marufuku hiyo imeanza leo saa sita usiku ambapo maeneo hayo yatakuwa katika zuio kwa siku 30.

Kutokana na hatua hiyo, kwa sasa hakuna usafiri wa barabarani,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kuondoka katika sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga kubwa la virusi vya corona.

“Ukiwapima Corona Wakenya 100, basi 20 watapatikana na virusi hivyo. Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi,”amesema Rais Uhuru Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta. (Picha na Ikulu).

Pia Rais Kenyatta ameamrisha kusitishwa mahudhurio ya wanafunzi madarasani katika vyuo vyote ikiwemo vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya ufundi. Ila tu kwa wale wanaofanya mitihani ya mwisho ya kumaliza masomo na wale katika vyuo vya afya hadi tamko litakapotolewa.
 
Hataua hiyo inaenda sambamba na kusitishwa kwa shughuli zote za michezo ikiwemo ile inayoendeshwa na wanachama wa vilabu nchini humo.

Rais Uhuru Kenyatta pia ametoa amri ya kusitishwa biashara za kwenye baa katika kaunti hizo zilizoathiriwa kuanzia.

Aidha,uuzaji wa pombe katika maeneo ya migahawa katika kaunti tano umepigwa marufuku. Na pia migahawa katika maeneo hayo hivi sasa yatauza vyakula na wateja watakiwa kuvichukua majumbani na siyo kula ndani ya migahawa.

Migahawa katika maeneo mengine ya nchi itaendelea kutoa huduma kama kawaida kwa kufuata miongozo ya afya ya umma nchini Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news