Rais Samia atangaza Baraza la Mawaziri wizara 23

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Machi, 2021 amefanya uteuzi wa Wabunge 3 na kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo amewabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri na ameteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai, mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 

Mhe. Rais Samia amefanya uteuzi wa Wabunge 3 ambao ni;

1.Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi)

2.Mhe. Balozi Liberata Mulamula

3.Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk

Mhe. Rais Samia amemteua Mhe. Balozi Hussein Athuman Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Balozi Katanga alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Baada ya mabadiliko, ifuatayo ni orodha ya Baraza la Mawaziri.

Ofisi ya Rais.

1Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Waziri – Mhe. Ummy Ali Mwalimu

(Kabla ya uteuzi huu alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira).

Naibu Mawaziri – Mhe. Dkt. Festo John Dugange

Naibu Waziri - Mhe. David Silinde

2.Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Waziri – Mhe. Mohammed Omar Mchengerwa

Naibu Mawaziri – Mhe. Deogratius Ndejembi

Ofisi ya Makamu wa Rais.
 

3.Muungano na Mazingira

Waziri – Mhe. Selemani Jafo

(Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa TAMISEMI)

Naibu Waziri – Mhe. Hamad Hassan Chande

Ofisi ya Waziri Mkuu.
 

4.Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Waziri – Jenister Joakim Mhagama

Naibu Mawaziri – Mhe. Patrobas Katambi

Naibu Waziri - Mhe. Ummy Nderianan
 

5.Uwekezaji

Waziri – Mhe. Geofrey Mwambe (Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara)

Naibu Waziri – Mhe. William Tate Ole Nasha

6.Wizara Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri – Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria)

Naibu Waziri – Mhe. Hamad Yussuf Masauni

7.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Waziri – Mhe. Elias Kwandikwa

8.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri – Mhe. Balozi Liberrata Mulamula

Naibu Waziri – Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk

9.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri – Mhe. George Simbachawene

Naibu Waziri - Mhe. Khamis Hamza

10.Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Waziri – Mhe. Leonard Chamriho

Naibu Waziri – Mhe. Geofrey Kasekenya

Naibu Waziri - Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara

11.Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri – Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Uwekezaji)

Naibu Waziri – Mhe. Exaud Kigahe

12.Wizara ya Madini.

Waziri – Mhe. Dotto Mashaka Biteko

Naibu Waziri – Mhe. Shukrani Manya

13.Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri – Mhe. William Lukuvi

Naibu Waziri – Mhe. Dkt. Angelina Mabula

14.Wizara ya Maji

Waziri – Mhe. Jumaa Hamidu Aweso

Naibu Waziri – Mhe. MaryPrisca Mahundi

15.Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

Waziri – Mhe. Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – Mhe. Pauline Gekul (Kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi)

16.Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Waziri – Mhe. Prof. Joyce Ndalichako

Naibu Waziri – Mhe. Omar Kipanga

17.Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Waziri – Mhe. Dorothy Gwajima

Naibu Waziri – Mhe. Godwin Mollel

Naibu Waziri – Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Waziri wa Fedha)

18.Wizara ya Nishati

Waziri – Mhe. Dkt. Medard Matogolo Kalemani

Naibu Waziri – Mhe. Stephen Byabato

19.Wizara ya Maliasili na Utalii.

Waziri – Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro

Naibu Waziri – Mhe. Mary Francis Masanja

20.Wizara ya Kilimo.

Waziri – Mhe. Prof. Adolf Mkenda

Naibu Waziri – Mhe. Hussein Mohammed Bashe

21.Wizara wa Mifugo na Uvuvi.

Waziri – Mhe. Mashimba Mashaka Ndaki

Naibu Waziri – Mhe. Abdallah Khamis Ulega (Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo)

22.Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Waziri – Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile

Naibu Waziri - Mhe. Kundo Mathew

23.Wizara ya Katiba na Sheria.

Waziri – Mhe. Prof. Palamagamba Aidan Kabudi (Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki)

Naibu Waziri – Mhe. Geofrey Mizengo Pinda

Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na waliobadilishiwa wizara wataapishwa kesho saa 9:00 Alasiri Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Aidha, Mhe. Rais Samia ametoa miezi 3 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Naibu Waziri wake kuanzisha wizara hiyo vinginevyo watahesabiwa kuwa wameshindwa kufanya majukumu yao.

Mhe. Rais Samia amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwamba watakaoshindwa kutimiza wajibu wao hatosita kufanya mabadiliko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news