Rais Samia kupokea ripoti ya CAG na TAKUKURU Ikulu ya Chamwino leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Machi Machi, 2021 atapokea taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20 na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/20, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Hafla ya kupokea taarifa hizo itafanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma na tukio hilo litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Chamwino.

Post a Comment

0 Comments