Serikali yatoa fursa kubadilisha tahasusi kwa Kidato cha Nne 2020

Serikali imewapa fursa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2020 kufanya mabadiliko ya machaguo ya tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali walizozichagua kupitia fomu ya Selform kuanzia leo Machi 29 hadi Aprili Mosi, 2021,anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).

Akizungumza na waadishi wa habari leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko ya tahasusi ni kuwawezesha wanafunzi kubadilisha machaguo yao kulingana na ufaulu wao kwenye matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne.

Waziri Jafo anafafanua kuwa, Serikali imetoa fursa kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kuwawezesha wanafunzi kusoma fani au tahasusi itakayowandaa kuwa na utaalam katika maisha yao

"Baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika tahasusi au kozi kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo waliyachagua, hivyo kwa sasa wanafahamu masomo waliyofaulu vizuri na wanaweza kuchagua tahasusi au fani za kusomea,”amesisistiza Waziri Jafo.

Hata hivyo, Waziri Jafo amesema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kumekuwa na uhitaji wa wataalam wa fani mbalimbali viyo Serikali imeanzisha tahasusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato cha tano mwaka huu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini.

Amezitaja tahasusi hizo kuwa ni Physics,Mathematics na Computer Studies (PMC),Kiswahili, French,Chinese (KFC),Kiswahili,English ,Chinese (KEC),Physical education,Biology,Fine art (PBF) na Physical education, Geography, Economics (PGE). 

Waziri Jafo amesema tahasusi ya PMC itatolewa katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Dodoma na Shule ya Sekondari ya wavulana ya Iyunga KFC na KEC itatolewa katika Shule ya Sekondari ya wasichana Morogoro na ya wavulana Usagara na tahasusi ya PBF na PGE itatolewa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Makambako, Shule ya Sekondari ya wavulana Kibiti na Sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.

"Nchi yetu ilikosa kuwa na wataalam wa Michezo kutokana na kutokuwepo na tahasusi maalum,hivyo hili ni jambo jipya ambalo mwanzo halikuwepo," amesisitiza Waziri Jafo


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news