TAARIFA MAALUM KWA MADEREVA WOTE WA MABASI, MALORI, TAXI, BODABODA, BAJAJI NA DALADALA

Kutokana na msiba Mkubwa uliolikumba Taifa letu la kuondokewa na Kiongozi makini aliyethubutu kuitoa nafsi yake kwa ajili ya kuwapigania wanyonge!
Madereva wote Tanzania mnaombwa siku ya kesho tarehe 26/03/2021, ule muda utakaotangazwa wa kushusha rasmi jeneza la mpendwa wetu Dr. John Pombe Magufuli, kila mmoja atakapokuwa hata kama upo na abiria Barabarani! Tunaomba usimame pembeni kwa dakika tano (5) tu. Ili kutoa heshima za mwisho, kisha uendelee na safari yako.

Imetolewa na: KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA MADEREVA TANZANIA TDF.

Post a Comment

0 Comments