Taifa Stars yaichapa Libya 1-0, yakwama kufuzu AFCON

Timu ya Taifa, (Taifa Stars) imekamilisha mechi zake za Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Ushindi huo wa leo Machi 28, 2021 umepatikana baada ya kuwavurumusha wageni hao kwa bao hilo katika dimba la Benjamin Mkapa lilopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Sallaam.

Kiungo mshambuliaji wa Wydad Club Athletic ya Morocco, Simon Msuva ndiye aliyewapa shangwe Watanzania baada ya kufunga bao hilo ndani ya dakika ya 45.

Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo Taifa Stars haijafuzu AFCON kufuatia kuzidiwa nguvu na Tunisia ikiwemo Equatorial Guinea zinazoshika nafasi mbili za kwanza na kukata tiketi ya kwenda Cameroon 2022.

Aidha, Tanzania inamaliza nafasi ya tatu kwa alama zake saba, nyuma ya Equatorial Guinea yenye alama tisa, Tunisia alama 16, wakati Libya ina alama tatu tu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news