Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today March 29th, 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 29/03/2021
......................
Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
....................
Mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara, Dar es salaam, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Kilimanjaro, Arusha na Manyara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........................
Mikoa ya Dodoma na Singida: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............................
ANGALIZO
VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA NJOMBE, IRINGA, RUKWA, SONGWE, MBEYA, RUVUMA NA KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 31/03/2021: Mabadiliko kidogo
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 29/03/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments