Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today March 30th, 2021

 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 30/03/2021.

.........................
Mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kigoma na Katavi: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
.........................
[Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro,Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara,Tabora
Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa na Rukwa: Inatarajiwa kuwa na
Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...........................
Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Ruvuma, Dodoma na Singida: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
KIWANGO CHA JUU CHA JOTO NI NYUZI JOTO 33 ( 32°C ) KATIKA MJI WA SAME.
..........................
ANGALIZO
1. VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA MWANZA,
KAGERA, GEITA, MARA, SIMIYU, SHINYANGA, KIGOMA NA KATAVI.
2. VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO
YA UKANDA WA PWANI YOTE YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA MTWARA, LINDI, DAR-ES-SALAAM,
TANGA NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA), PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA).
 
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.
Matarajio kwa siku ya Alhamisi tarehe 01/04/2021: Mabadiliko kidogo
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 30/03/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news