Watu Bilioni 3.9 washuhudia mwili wa Hayati Dkt.Magufuli ukiagwa jijini Dodoma

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu Bilioni 3.9 Duniani kote wamefuatilia tukio la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla ya kuaga mwili wake iliyofanyika Machi 22, 2021 jijini Dodoma ambako tukio hilo lilikuwa la kitaifa, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa ameyasema hayo Machi 23, 2021 jijini Zanzibar wakati akiwahutubia wananchi katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.Magufuli jijini humo.

“Kwa taarifa tulizonazo mpaka jana jioni zaidi ya watu Bilioni 3.9 karibu watu Bilioni 4 Duniani walikuwa wanafuatilia tukio la kumuaga Hayati Magufuli Kitaifa jana Dodoma na ninaamini leo pia itakuwa hivyo,"ameeleza.

Majaliwa amesema kuwa,wataendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukamilisha yale aliyayaanzisha Hayati Dkt.Magufuli wakati wa uhai wake.

“Kwa niaba ya Kamati ya Mazishi Kitaifa bado tuko kwenye siku za huzuni tangu siku tumetangaziwa kifo cha Rais wetu mpendwa, ni tukio lisilo la kawaida sana kuondokewa na Rais akiwa madarakani, ila ni mipango ya Mungu na sisi viongozi tunaahidi kuendeleza Ilani na kutekeleza na kukamilisha yale aliyoyaanzisha,”amesema.

Post a Comment

0 Comments