WAUMINI WA MASJID RAUDHWA WAHOFIA UCHAGUZI

Waumini wa msikiti wa Raudhwa uliopo Jijini Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa msikiti huo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 20 Machi Mwaka huu, anaripoti Danson Kaijage (Mwanza).
Sababu za waumini kuomba serikali kuzuia uchaguzi huo ni madai kwamba mwenendo wa uchaguzi huo unaendeshwa kinyume na katiba ya waumini wa msikiti huo.

Inaelezwa kuwa Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini ( RITA ) imeingilia uchaguzi wa msikiti huo na kuwafanya waumi wenye msikiti na mali zao kutokuwa na sauti ya kufanya maamuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na DIRAMAKINI wamesema kuwa kuna mpango wa kufanya uchaguzi, lakini uchaguzi huo umeghubikwa na sintofahamu.

Mohamed Bakarani 65 ambaye naye ni mgombea katika uchaguzi huo wa Bodi ya wadhamini katika msikiti wa Raudhwa amesema kuwa mwenendo wa ugawaji wa fomu za uchaguzi zinazotolewa na RITA bado haujakaa sawa.

Bakarani amesema kuwa kinachoshangaza ni jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendeshwa Kwa kuwanyima waumini wa msikiti huo maamuzi kwa mujibu wa katiba na sheria wa lizojiwekea.

"Mimi ni mmoja wa wagombea nafasi ya ujumbe ww bodi ya udhamini na mpaka sasa waliochukuwa fomu watu 50 lakini nimeuliza je nani atachambua majina ya wagombea ili kurejesha majina 14 yanayotakiwa ili yapigiwe kura?

"Najaribu sasa kuuliza je serikali inawajua vyema waumini wa msikiti wa Raudhwa ambao wamechukua fomu na ni kwanini iwe RITA baada ya kuwaacha waumini kufanya kazi hiyo kutokana kuwa ni wazi waumini wanauelewa mpana wa kiutendaji kwa waumini wenzao.

"Pia naniuliza hawa RITA wanataka kufanya uchavuzi kwa katiba gani ya wao au ya msikiti maana ya msikiti ndiyo iliyopo mambo ya ndani ya nchi iliyofanyiwa marekebisho ambayo kwa sasa wanaikataa na kutaka kutumia ya zamani ambayo ilishapitwa na wakati"amesema Barakani.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi kamati ya mpito Msikiti wa Raudhwa Jijini Mwanza,Chasa Yahaya Mongela amesema chaguzi haitakuwa huru na haki kutoka na kuingiliwa zaidi na RITA.

Amesema kuwa mgogoro wa msikiti wa Raudhwa ni wa muda mrefu na wanaokwamisha ni watu wa RITA kwa kuweka masilahi yao binafsi badala ya kuangalia maslahi ya waumini wa Msikiti huo.

Kutokana na hali hiyo Mongela amesema waumini wa msikiti huo hawapo tayari kufanya uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa bodi ya wadhamini kutokana na mchakato unaoendelea kutoeleweka.

"Ikumbukwe kuwa bodi ya wadhamini ilivunjwa kutokana na kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha na wapo baadhi ya wajumbe walirejeshwa kazini kinyume na taratibu.

"Cha kushangaza mjumbe ambaye aliondolewa kwenye bodi kwa tuhuma ya ubadhilifu na kupisha uchunguzi alirudishwa kwa mlango wa nyuma na akaendelea kuwa mhasibu pamoja na kuwa iliundwa kamati ya uchunguzi lakini mpaka sasa hakuna mrejesho ambao waumini wamepewa.

"Kuhusu uchaguzi wa Bodi ya wadhamini wa mali za msikiti wa Raudhwa haijulikani ni katiba gani inatumika maana katiba ya waumini imepigwa chini na sasa inasemekana itatumika katiba mama ya RITA,"ameeleza Mongela.

Kwa upande wake Ofisa wa RITA ambaye anagawa fomu za mugombea aliyepo Jijini Mwanza,Haidary Adam,amesema kuwa kinachofanyika ni kufanya uchaguzi kwa Mujibu wa katika ya RITA kwa kutumia sheria mama.

"Pamoja na kusema kuwa waumini hawatafanya uchaguzi lakini tulikaa na waumini wote wa Msikiti Raudhwa na kuwahakiki kwa idadi ya waumini 224 na majina yao kubandikwa kwenye mbao za Matangazo kwa uhakiki zaidi.

"Kuhusu katiba ya waumini na katiba nyingine ilionekana katiba zao zinamapungufu na kutokana na hali hiyo tulikubaliana kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba ya RITA kwa kutumia sheria mama ya bodi ya udhamini,"ameeleza Adam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news