Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro kumaliza mgogoro Kitalu cha Uwindaji Lake Natron

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya kikao cha pamoja na Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Green Mile Safari Company Ltd (GMS) kufanya mapitio ya uamuzi wa kuifutia umiliki wa kitalu cha Lake Natron kilichopo Wilayani Longido mkoani Arusha, anaripoti Lusungu Helela (WMU) Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dodoma na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Mkuu wa Wilaya hiyo, wananchi na waandishi wa habari kwa lengo la kusikiliza pande zote zinazoguswa na suala la kufutwa kwa leseni ya kitalu hicho
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha mapitio ya uamuzi uliofanyika wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron (East) kilichopo wilayani Longido, Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) kufuatia kampuni hiyo kuwasilisha maombi ya kufanyia mapitio uamuzi uliotolewa awali kwa mujibu wa Kifungu cha 38(14) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009. Kikao hicho cha wazi kimehudhuliwa na baadhi ya Watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Viongozi wa Wilaya ya kutoka Halmashauri Longido na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akitoa utaratibu wa namna atakavyoendesha kikao cha mapitio ya uamuzi wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron (East) kilichokua kikimilikiwa na Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) wilayani Longido, leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao cha kufanya mapitio ya uamuzi uliotolewa na Serikali mwaka 2019 wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) kilichopo wilayani Longido. Viongozi wa Kampuni hiyo walitoa utetezi wao mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Maurus Msuha akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Lucy Saleko wakifuatilia utetezi uliokuwa ukitolewa na viongozi wa kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Green Mile Safari mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii, leo Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Eblate Mjingo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki ( kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kushoto) wakifuatilia utetezi wa kampuni ya uwindaji wa Kitalii ya Green Mile Safari mbele ya ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro kwenye kikao cha maombi ya kufanya mapitio ya uamuzi wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron (East) cha Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) kilichopo wilayani Longido leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe akijibu baadhi ya maswali kwenye kikao cha maombi ya kufanyika mapitio ya uamuzi wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron (East)cha Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) leo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Longido, Dkt. Steven Kiruswa akizungumza mara baada ya Kampuni ya Green Mile Safari iliyokuwa ikimiliki kitalu cha Uwindaji cha Lake Natron ( East) kutoa utetezi katika kikao cha wazi kilichokua kikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wengert Windrose, Abdulkadiri Mohammed akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali wakati wa kikao cha kufanya mapitio ya uamuzi uliotolewa mwaka 2019 wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii, Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Green Miles Safari, Awadhi Abdala akisikiliza baadhi ya maswali aliyokuwa akiulizwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa kikao cha kufanyika mapitio ya uamuzi wa kuifutia umiliki wa Kitalu cha uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron (East) cha Kampuni ya Green Mile Safari (GMS) kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

Leseni ya Kitalu hicho ilifutwa mwaka 2019 na Waziri mwenye dhamana ya Maliasili kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 38 (12) cha sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009. Kufuatia kufutwa kwa umiliki huo, GMS iliwasilisha maombi ya kufanyika kwa mapitio ya uamuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 38 (14) cha sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.

Aidha, baada ya kupokea maombi ya kufanya mapitio na kusikiliza pande zote, Dkt. Damas Ndumbaro ameahidi kufika katika eneo la kitalu kilichofutiwa umiliki wilayani Longido ili kujionea hali halisi na baadae kufanya maamuzi kuhusu maombi ya kurejeshewa Kitalu hicho yaliyowasilishwa na Kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro lengo la kufika katika eneo hilo la kitalu ambacho leseni yake imefutwa ni kujionea hali halisi kuwezesha maamuzi kutolewa.

Post a Comment

0 Comments