WHO yatoa wito kwa Dunia kuchangia chanjo ya Corona

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa Dunia kuchangia chanjo ya kuzuia virusi vya Corona (COVID-19) kwa nchi zenye kipato cha chini.
Tedros Adhanom Ghebreyesus | WHO / VIA REUTERS

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao kutokea mjini Geneva, Uswisi akisema kuwa zinahitajika dozi milioni 10 katika program ya chanjo inayosimamiwa na shirika hilo.

Dkt.Tedros amesema, COVAX ipo tayari kusambaza chanjo, lakini hiana dozi za kutosha kutekeleza mpango huo.

COVAX ni programu ya usambazaji chanjo ya Covid-19 duniani yenye lengo la kuhakikisha Dunia inafikia chanjo na hasa katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

Miongoni mwa mambo ambayo WHO imeomba pia ni kuhakikisha programu ya COVAX inafadhiliwa ili iweze kusambaza chanjo katika nchi husika kwa wakati.

Hadi sasa kupitia programu ya COVAX zaidi ya dozi milioni 31 za chanjo zimesambazwa katika nchi 57 duniani.

Post a Comment

0 Comments