WIZARA YA MADINI KUWAJENGEA UELEWA WA SHERIA YA MADINI KAMPUNI YA SHANTA

Waziri wa Madini Doto Biteko ameuagiza uongozi wa Wizara ya Madini kukutana na viongozi pamoja na wanasheria wa Kampuni ya Shanta ili kuwajengea uelewa juu ya Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika Sekta ya Madini,anaripoti Tito Mselem (WM).
Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto) akizungumza jambo kwenye kikao kati yake na viongozi wa Mgodi wa Shanta katika Ukumbi wa Utawala Chumba namba 31 uliopo Bungeni jijini Dodoma Machi 30, 2021, kulia ni Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya.
Hayo, ameyasema leo Machi 30, 2021 alipokutana na Kampuni ya Shanta kujadili suala la gawio la asilimia 16 linalotakiwa kutolewa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Biteko amesema, Kampuni ya Shanta ilete Wanasheria wake ili Wanasheria wa Wizara watoe mafunzo na maelekezo ya Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika Sekta ya Madini.

Aidha, Waziri Biteko amesema, tumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ndoto zake za kufungua kwa wingi migodi ya uchimbaji wa madini ili Nchi iweze kuwanufaisha watanzania.

Pia, Waziri Biteko amewataka viongozi wa Kampuni ya Shanta kuhakikisha wanaanza kazi ya uzalishaji haraka ili waweze kusaidia wananchi wanaozunguka eneo hilo ikiwemo upatikanaji wa ajira kwa watanzania.

Vilevile, Waziri Biteko ameutaka uongozi wa Kampuni ya Shanta kutoa gawio la Serikali la asilimia 16 kwa mujibu wa Sheria ya Madini inavyoelekeza.

Awali, Waziri Biteko, alimpongeza aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwa kuteuliwa na kupigiwa kura na wabunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news