Diamond Platnumz ndiye Balozi wa Itel, kulipwa mabilioni ya fedha

Kampuni ya itel inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki imemlipa mabilioni ya pesa msanii maarufu Afrika Diamond Platnumz ili kuwa balozi wake.

Katika taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa instagram katika page ya itel Tanzanzania imeeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha Diamond Platnumz kuwa balozi wa itel.

“Leo ni siku maalum! Tunayo furaha kubwa kumkaribisha Diamond Platnumz balozi wetu mpya wa itel.” Imesema sehemu ya chapicho hilo.
Moja ya post iliyopostiwa ukurasa wa instagram @iteltanzania yenye picha ya Diamond akiwa ameshika simu ya itel A37.

Japo kiwango halisi alicholipwa hakijatajwa, lakini ukurasa wa instagram wa wasafi TV umechapisha taarifa kuwa kampuni ya itel imemlipa Diamond Platnumz mabilioni ya pesa.

“Staa wa Muziki Barani Afrika @diamondplatnumz, amelamba dili jingine kubwa na nono, baada ya kutangazwa kuwa Brand Ambassador (Balozi) wa vifaa vya kampuni ya #Itel @iteltanzania .

Kwa mujibu wa Source yetu, Dili hili linaweza kuwa Moja ya Dili kubwa zaidi @diamondplatnumz kuwahi kupata, kwasababu linajumuisha Afrika nzima na limehusisha Mabilioni ya fedha .” imeeleza sehemu ya chapisho la taarifa hiyo.
Kwa upande mwingine Diamond amethibitisha katika chapisho lake la ukurasa wa instagram kuwa sasa ni rasmi amekuwa balozi wa itel.

“Nina furaha kuwajuza kuwa, sasa ni Balozi wa Bidhaa za itel” imesema taarifa hiyo.
Post aliyotumia Diamond Platnumz kutangaza kuwa sasa ni balozi wa itel.

Kwa Taarifa zaidi tembelea kurasa za itelTanzania instagram na Facebook au bofya hapa: https://www.instagram.com/iteltanzania/

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news