Hawa ndio madereva 10 wa mabasi mikoani waliofungiwa na Waziri Simbachawene leo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewafungia kwa muda wa miezi mitatu madereva 10 wa mabasi ambao wamekuwa wakikiuka sheria ya usalama barabarani kwa kuendesha mabasi yao kwa mwendo kasi, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).

Pia, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva hao ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani kwa makosa hayo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma leo, ambapo ametangaza majina kumi ya madereva waliofungiwa kuendesha mabasi kutokana na ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Uamuzi huo ameufikia leo Aprili 1, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma huku akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Khamisi Hamza Chilo.

Waziri Simbachawene amewataja madereva hao kuwa ni Allan Msangi ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T605 DJR kutoka Kampuni ya Kapricon ambalo hufanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Moshi na hutembea kwa kilomita 125 kwa saa.

Waziri huyo amemtaja dereva mwingine ni Hussein Dudu kutoka kampuni ya Kimotco Intertrade ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T520 CXE ambalo hufanya safari katika mikoa ya Arusha na Musoma na hutumia mwendokasi wa kilomita 126 kwa saa.

Waziri Simbachawene amemtaja dereva mwingine kuwa ni Selemani Selemani ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 313 DSO kutoka kampuni ya Al Saedy ambalo hufanya safari zake katika njia ya Dar es Salaam,Kilombero na hutumia mwendokasi wa kilomita 103 kwa saa.

Amemtaja dereva mwingine ni Athumani Mzava ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 391 kutoka kampuni ya MB Coach ambalo hufanya safari zake katika njia ya Dar es Salaam,Arusha na hutumia mwendokasi wa kilomita 107 kwa saa.

Waziri Simbachawene amemtaja dereva mwingine ni Juma Simba ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 340 DPW kutoka Kampuni ya Baraka Classic ambalo hufanya safari zake katika maeneo ya Dar es Salaam,Masasi na hutumia mwendokasi wa kilomita 107 kwa saa.

Amemtaja dereva mwingine ni Salum Salum ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 121 DEA kutoka Kampuni ya Maning Nice ambalo hufanya safari zake Dar es Salaam ,Tunduma na hutumia mwendokasi wa kilomita 110 kwa saa.

Waziri Simbachawene amemtaja dereva mwingine ni Frank Masawe ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 694 DRB kutoka kampuni ya Machinga ambalo hufanya safari zake katika mikoa ya Dar es salaam,Mtwara na hutumia mwendokasi wa kilomita 95 kwa saa.

Amemtaja dereva mwingine ni Innocent Thomas ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 225DTB kutoka kampuni ya Ester Luxury ambalo hufanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam,Moshi na hutumia mwendokasi wa kilomita 107 kwa saa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma leo, ambapo ametangaza majina kumi ya madereva waliofungiwa kuendesha mabasi kutokana na ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani).

Waziri Simbachawene amemtaja dereva mwingine ni Nassib Nasoro ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 565 BED kutoka kampuni ya NBC Classic ambalo hufanya safari zake katika mikoa ya Tabora na Kigoma na hutumia mwendokasi wa kilomita 109 kwa saa.

Pia amemtaja dereva mwingine ni Maiko Mkindi ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 675 DHY kutoka kampuni ya Kilimanjaro Express ambalo hufanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha na hutumia mwendokasi wa kilomita 100 kwa saa.

“Kwa mamlaka niliyonayo nawafungia madereva hawa kwa muda wa miezi mitatu.Nawaagiza wamiliki wa mabasi haya ambayo madereva wamekiuka sheria ya usalama barabarani kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa madereva wao,”amesema Waziri Simbachawene. Vilevile aliliagiza Jeshi la Polisi kuwapeleka Mahakamani madereva hao ili iwe fundisho kwa wengine.

Post a Comment

0 Comments