Jaji mstaafu Dkt.Bwana: Tume imetoa uamuzi wa rufaa 151 na malalamiko 11 yaliyowasilishwa na Watumishi

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, leo amehitimisha Mkutano wa Tume namba 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 uliofanyika Jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana amesema, katika Mkutano huu Tume imetoa uamuzi wa Rufaa 151 na Malalamiko 11 yaliyowasilishwa na watumishi mbalimbali wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Mamlaka zao za Ajira na Mamlaka za Nidhamu.

Kati ya rufaa 151 zilizotolewa uamuzi na Tume rufaa 82 zimekataliwa; rufaa 43 zimekataliwa kwa kuwa ziliwasilishwa nje ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Rufaa 12 zimekubaliwa; rufaa 11 zimekubaliwa kwa masharti kwamba zikashughulikiwe upya na Mamlaka zao za Nidhamu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Rufaa 3 hazikutolewa uamuzi kwa sababu ni kesi zilizopo Mahakamani.

Kwa upande wa malalamiko, Tume ilipokea na kutoa uamuzi wa malalamiko 11 ambapo malalamiko 6 yamekataliwa, malalamiko 4 yamekubaliwa na lalamiko 1 limekataliwa kwa sababu liliwasilishwa nje ya muda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news