Mabilionea kutoka Falme za Kiarabu kuwekeza kiwanda cha dawa za binadamu Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ipo tayari kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza nchini katika sekta tofauti ili kukuza uchumi wa Zanzibar, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Ahmed Nassor Mazrui wakati alipokutana na ugeni wa kampuni ya Afri amco kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo imekusudia kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu hapa nchini.

Amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya itahakikisha inawapa fursa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ya Afya ili kuboresha na kuimarisha huduma zinazotolewa.

Ameeleza kuwa uwekezaji huo utawanufaisha wananchi wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na ajira na wanafunzi kupata mafunzo kwa njia ya vitendo vya utengenezaji na upatikanaji wa dawa kwa urahisi.

Nae Meneja mkuu wa kampuni ya Afri amco and Mglory Holding Limited, Mhandisi Khalid Mohamed Abubakar amesema wanashauku kubwa ya kuwekeza kiwanda cha kuzalisha dawa hapa nchini kwani kutasaidia kupunguza gharama ya uagizaji kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa, dawa ambazo zizozalishwa zitauzwa ndani na nje ya nchi hali ambayo itarahisisha upatikanaji wa dawa kwa bara la Afrika.

Kampuni ya Afri amco ambayo makao yake yapo Umoja wa Falme za Kiarabu ina uhusiano wa karibu na Nchi ya China, India na pia imejikita katika nchi 17 katika bara la Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news