MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWATEMBELEA WATOTO YATIMA, WAZEE NA WENYE MAHITAJI MAALUM DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Ali Mwaka (1) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati Makamu wa Rais alipofika katika Kituo hicho leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha taslimu kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Gilbert Mezi ( 11) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati Makamu wa Rais alipofika katika Kituo hicho leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Gilbert Mezi ( 11) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati alipofika katika Kituo hicho leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji Watoto, Wazee na Watu wenye Mahitaji Maalum wanaotunzwa katika Kitu hicho ikiwa ni maadhimisho ya Jumaatatu ya Pasaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango wakiwaangalia Watoto wanaolelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati walipotembelea katika Kituo hicho leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka. kushoto ni Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akikabidhi Vifaa mbalimbali ikiwemo Chakula na Vinywaji, Fedha Jumla ya Shilingi Milioni Tano kwa Sister. M. Prodencia M. C wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma, kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka kwa Watoto Yatima, Wazee na Watu wenye Mahitaji Maalum wanaotunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma leo April 5,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza jambo na Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas, baada ya kumalizika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka leo April 05,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango, Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kumalizika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka leo April 05,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango wakiwa katika Picha ya Pamoja na Watoto, Wazee pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum, wakati walipowatembelea katika Kituo chao cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.

Post a Comment

0 Comments