Nabii Joshua: Kampeni ya Kuliombea Taifa inaendelea

Rais wa New Covenant Unity International (NCUI) ambaye pia ni Kiongozi wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala amesema kuwa, Kampeni ya Kuombea Taifa (Pray for Nation) ambayo imewafikia mamilioni ya Watanzania katika mikoa mbalimbali nchini inaendelea, anaripoti Mwandishi WETU, Mikumi.
Ameyasema hayo baada ya kufungua rasmi kituo cha Sauti ya Uponyaji Tanzania maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa kupanua huduma ya kuhubiri injili kwa Watanzania wote bila kujali dini, kabila au rika.

"Mungu wetu ni mwema sana, hii ni hatua njema ya kuhakikisha tunaendelea kuhubiri habari njema ili kuwaleta watu kwa Mungu, watu waweze kulifahamu vema kusudi la Mungu kwao ili waweze kuishi kwa upendo, amani na mshikamano.
"Uzinduzi huu wa leo unawezesha kuvuka makanisa zaidi ya 100 vijijini na mijini ambayo nimekuwa nikiyasimamia sasa na ninaamini kuwa, Mungu wetu kupitia madhabau hii anakwenda kuwaponya wenye shida mbalimbali, kuwapa faraja waliokata tamaa na kuzipa amani familia ambazo zilikuwa zimehitilafiana, vivyo hivyo kuliombea Taifa letu ili upendo na amani izidi kustawi zaidi. Niseme tu kwamba ile Kampeni ya Kuliombea Taifa yaani Pray for Nation ambayo niliianzisha miaka kadhaa iliyopita inaendelea. Muda wowote kuanzia sasa nitatangaza ratiba ya wapi tutaanzia,"amesema Nabii Dkt.Joshua.

Mbali na hayo amesema kuwa, ataendelea kuandaa makongamano mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha umoja na kudumisha amani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuongoza maombi ya kuombea Taifa na Dunia kwa ujumla.
"Na hayo yataenda sambamba na kuwapa faraja watu ambao wanapitia hali ngumu za kimaishama, yatima,wajane,walemavu na wagonjwa kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali na maombi pia. Katika makongamano hayo ninaamini wengi watapokea uponyaji na majawabu ya mahitaji yao kutoka kwa Mungu,"amesema Nabii Joshua.

Wakati huo huo,Nabii Dkt.Joshua amesema kuwa, ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi mbalimbali za maendeleo vijijini na mijini chini ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Nimekuwa mdau wa maendeleo na nitaendelea kufanya hivyo kwa kutoa misaada ya umeme jua kwenye vituo vya afya vijijini,kujenga na kukarabati madarasa ya baadhi ya shule za misingi kama niivyofanya awali,”amesema Nabii Dkt.Joshua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news